24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

TECNO Yagusa Hisia: Mchezo wa Hisani wachochea hamasa ya kuboresha viwanja vya jamii Barani Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kama mdhamini rasmi wa Kombe la  (AFCON) Afrika nchini Ivory Coast, kampuni ya teknolojia , TECNO iliandaa mechi ya hisani iliyojaa nyota magwiji wa mpira wa miguu Africa siku ya pili ya sherehe ya ufunguzi.

Mechi hiyo ilishirikisha Katibu Mkuu wa CAF, Véron Mosengo-Omba, wachezaji maarufu wa mpira akiwemo Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf, Asamoah Gyan, Dennis Oliech na Erick Otieno, waliyoonyesha ushirikiano wao kwa michezo na maendeleo ya jamii.

Picha ya pamoja Timu ya CAF Pamoja na magwiji wa Soka Afrika.

Kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki, TECNO ilitangaza mpango wa kufadhili matengenezo ya viwanja 100 vya mpira vya jamii zote Afrika ndani ya miaka mitano ijayo. Mpango huu unalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana, kukuza maisha yenye afya na kuhakikisha upatikanaji wa viwanja bora vya michezo katika jamii zisizopewa kipaumbele.

Meneja Mkuu wa TECNO, Jack Guo, alisema kwa hamasa, “Tumeanzisha safari ya kuzitia mwangaza ndoto zisizohesabika kwa kuboresha viwanja 100 kote Afrika,” akisisitiza nguvu ya kubadilisha ya mpango wa TECNO. Taylan Tankpinou, mvulana wa miaka 10, aliongeza, “Asante kwa TECNO, tunajenga maeneo bora ya kuchezea na kukua!

Hotuba ya Mpango wa Kifadhili.

Ili kuhamasisha zaidi, TECNO ilitangaza kwamba kwa kila goli lililofungwa katika mchezo huo liligharimu, dola 10,000 ambazo zingechangiwa kwenye kampeni hiyo.

Mchezo ulimalizika na TECNO kuchangia dola $50,000 zaidi kwa mradi huo. Ahadi hii ilifanya kila goli kuwa shangwe si tu kwa wachezaji bali pia kwa vizazi vijavyo ambavyo vitafaidika na miundombinu bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles