29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Misri yaipongeza Tanzania kwa kutekeleza mradi wa JNHPP

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nyumba, Nishati na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Assim Elgazzar ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao umefikia asilimia 95.83 hadi sasa.

Waziri huyo ametoa pongezi hizo Januari 22, 2024 mara baada ya kutembelea Mradi huo uliopo Rufiji katika mkoa wa Pwani akifuatana na mwenyeji wake, Naibu Waziri wa Nishati wa Tanzania, Judith Kapinga.

Amesema Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Mradi huo wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere ambao utasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme nchini Tanzania.

“Maendeleo ya utekelezaji wa mradi huu ni mazuri na ndani ya muda mfupi ujao tunatarajia kuona mradi huu ukikamilika na kumaliza kabisa changamoto ya umeme hapa Tanzania,” amesema Elgazzar.

Amesema Serikali ya Misri inataka kuona mradi huo ukikamilika kwa wakati na ufanisi mkubwa ambapo Misri itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakandarasi katika hatua zote za utekelezaji wa Mradi huo.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameeleza kuwa Waziri Elgazzar ametumwa na Rais wa Misri kwa ajili ya kuona maendeleo ya mradi huo ambao umefikia asilimia 95.83 na unajengwa na Kampuni ya JV Elsewedy na Arab Contractor kutoka Misri.

Wengine walioshiriki katika ziara hiyo ni Mkurungenzi mkuu wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles