23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

TCRA waeleza sababu za laini kusajiliwa upya

Derick Milton, Simiyu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema lengo la mfumo mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole (Biometric Registration) linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi waliosajili laini kwa kutumia vitambulisho feki.

Kutokana na hali hiyo, mamlaka imekuwa ikipata wakati mgumu katika kubiliana na vitendo vya kihalifu vinavyotokea kwa njia ya mtandao.

Hayo yamelezwa leo na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo, wakati wa kuzindua kampeni ya kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mfumo huo mkoani wa Simiyu.

“Kuanzia Mei Mosi mwaka huu, wananchi wote wanatakiwa kusajili laini zao kwa mfumo huo, na laini ambazo hazitasajiliwa zitafungiwa pindi tutakapotangaza muda wa ukomo.

“Tunatambua kwa kutumia mfumo huu, itaondoa udanganyifu mkubwa unaosababisha kuwepo kwa ugumu wa TCRA katika kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kutumia mitandao,” amesema Mhandisi Mihayo.

Aidha Mihayo amesema katika mfumo huo wananchi watatakiwa kwenda na kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho kwa ajili ya kusajili laini zao.

Akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kusajili laini zao upya kwa mfumo huo huku akiwataka kwenda na vitambulisho vya NIDA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles