25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Rais Macron aahidi kujenga upya Kanisa la Notre-Dame

Rais wa Ufaransa ameahidi usaidizi wa kimataifa katika kulijenga upya kanisa kongwe la Notre Dame mjini Paris baada ya sehemu ya kanisa hilo kuteketea na moto na kuharibika.

Maafisa wa zima moto walifanikiwa kuliokoa jengo hilo la historia lenye miaka 850 lakini paa na mnara wa jengo hilo yameanguka.

Moto huo ulidhibitiwa saa tisa baada ya kuanza.

Chanzo chake hakijajulikana lakini maafisa wanasema huenda ukahusishwa na ukarabati mkubwa unaoendelea.

Moto mkubwa ulizuka katika kanisa hilo kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa, jengo ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka.

Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na moto huku mwingine ukifanikiwa kuzimwa katika minara miwili ya kengele.

Wazima moto wanafanya kila juhudi kuokoa vito vya thamani vilivyoko ndani kanisa hilo na pia kuzuia mnara wa upande wa kaskazini kutoporomoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles