25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Tausi Likokola achangisha milioni 14 kusaidia albino

Taus LikokoNa Mwandishi Wetu
BAADHI ya fedha zilizokusanywa usiku wa Tausi uliofanyika katika Hoteli ya Coral Beach Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, zimeelekezwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kikundi cha Wamata na Kiwawede cha Mburahati ambacho kinatunza watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Usiku huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mwandishi mashuhuri, Jenerali Ulimwengu, mwanamitindo Mustafa Hasanali, aliyekuwa Miss Tanzania, Sitti Mtemvu na wengine wengi.
Ulisindikizwa na muziki uliongozwa na bendi ya Kalunde chini ya usimamizi wake, Ben Mwanambilimbi na mwongozaji wa shughuli hiyo alikuwa aliyewahi kuwa Mr. University, Matukio Chuma.
Shughuli hiyo iliendeshwa kwa wageni waalikwa kujitokeza mbele ya ukumbi kisha kutangaza kiasi wanachochangia kwa ajili ya kununua ‘Tausi perfume’ iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh 45,000 kwa moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles