Tundaman: Nipo tayari kuwasaidia vijana wa Manzese

0
1352

TUNDA MANNA JENNIFER ULLEMBO
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Ramadhan ‘Tundaman’, ameweka wazi kwamba yupo tayari kutoa msaada kwa vijana wanaoishi maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam.
Akifafanua kauli yake hiyo, alisema anatamani awe daraja la mafanikio kwa vijana hasa waliokata tamaa ya maisha ili awaongoze katika maisha mapya na ya matumaini.
“Nipo tayari kuwasaidia hata katika ushauri hasa vijana waliokata tamaa ya maisha wasisite waje nyumbani hata kama sitakuwepo, watakutana na wazazi wangu watawaelekeza nilipo maana nikifanya hivyo itasaidia sana kubadilisha fikra za vijana wengi wanaokimbilia kwenye dawa za kulevya, unywaji wa pombe na uvutaji wa bangi,” alisema Tundaman.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here