25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yapokea Sh bil 33 kwa ajili ya kilimo

Mwandishi Wetu- Dodoma

SERIKALI  ya Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wa Dinar milioni 4.5 sawa na Sh bilioni 33.9 kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFED) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji wa onde la Mto Luiche mkoani Kigoma.

Hayo yalismwa jijini Dodoma jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja.

Alisema  mkataba huo, umesainiwa nchini Kuwait kati ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Aisha Amour, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa KFED, Abdulwahad Ahmed Al- Bader, kwa niaba ya Serikali ya Kuwait.

“Fedha hizo za mkopo zitatumika katika uhakiki wa usanifu wa kina wa mradi na usimamizi wa ujenzi wa bwawa la maji la mita 375 lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo milioni 70 za maji”, alisema.

Alisema fedha hizo, pia zitatumika katika ujenzi wa miundombinu kama mifereji ya maji, kinga za mafuriko, daraja na barabara zitakazotumika kutoa huduma zenye urefu wa kilometa 21.

Alisema  mradi huo, unategemewa kuongeza wigo wa kilimo cha umwagiliaji kwa takribani eneo la hekta 3,000 na kutoa fursa za ajira mbalimbali kabla na baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi.

Zao ambalo linatarajiwa kuzalishwa eneo la mradi ni mpunga, linatarajiwa kuongeza kipato cha wakulima lakini pia kutekelezwa kwa dhana ya Serikali ya kuwa na kilimo cha kisasa kitakachoongeza usalama wa chakula nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles