25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania mbioni kuacha kuagiza vyakula vya watoto kutoka nje

MWANDISHI WETU-MOROGORO

TANZANIA  iko mbioni kuachana na kuagiza vyakula vya nyogeza kwa watoto kutoka nje ya nchi,matokeo yake vitaanza kuzalishwa  nchini,baada ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuja na mradi wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka mitano, ili kuhakikisha wanapata chakula kilichoboreshwa na kinachokidhi mahitaji yao.

Akizungumza mwishoni mwa wiki,  wakati wa uzinduzi wa mradi huo mkoani Morogoro,Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya  Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Edward Mbanga alisema hadi sasa hakuna hakuna uzalishaji wa kibiashara wa vyakula vya nyongeza hapa nchini na badala yake vimekuwa vikiagizwa kwa wazalishaji mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Alisema mradi huo ambao unafadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), utahusisha vyakula vya nyongeza vinavyopatikana nchini, ambavyo vimetajwa pia vitasaidia kuboresha matibabu ya Utampiamlo wa kadiri na vitatoa ajira kwa Watanzania watakaozalisha vyakula hivyo.

“Mradi huuu utakuwa msaada mkubwa kwa jamii,utengenezaji wa vyakula vya nyongeza kwa ajili ya Watoto chini ya miaka mitan utasiadia kuzuia na kutibu utapiamlo wa kadiri nchini, ni wazi vyakula vitakavyohusika ni vile ambavyo vinapatikana nchini,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Germana Leyna alisema   mradi huo utasaidia kuongeza upatikanaji rahisi wa chakula kilichotengenezwa ndani ya nchi kikiwa salama  kuweza kuwapatia watoto lishe bora.

Alisema vyakula hivyo vitaweza kupatikana kwa gharama nafuu na wameamua kufanya hivyo ili kuwezesha kila Mtanzania kumudu gharama zake na kuweza kumudu kukipata pindi atakapokihitaji.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Profesa Andrea Pembe ambaye ni washiriki pia kwenye mradi huo alisema suala la kuagiza vyakula vya nyongeza kutoka nje ya nchi kamwe halikubaliki hivyo kupitia mradi huu endapo utatekelezwa kama ulivyopangwa basi utasaidia kupunguza matatizo ya utampiamlo na udumavu kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, Juliana Muiluri alisema wamejitoa kuhakikisha unafanikiwa, endapo utafanyika kama ulivyokusudiwa basi utaweza kuitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa katika mapambano dhidi ya utapiamlo na udumavu.

 Mradi huo,utaenda sambamba na kutafiti kuhusu ufanisi na kukubalika kwa vyakula hivyo hivyo kupitia mradi huu kutatengenezwa bidhaa za chakula kwa makundi mengine ya watu  kama vile wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles