26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

TAWLA wasisitiza ushiriki kukabili mimba za utotoni

YOHANA PAUL, KISHAPU.

CHAMA Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Mkoa wa Mwanza, kimewashauri viongozi wa ngazi zote kuanzia mitaa, vijiji, kata   na halmashauri kushirikiana na kuweka dhamira ya pamoja ili kufikia adhima ya kudhibiti ndoa na mimba za utotoni.

Rai hiyo, ilitolewa juzi na Wakili na Mratibu wa TAWLA Mkoa wa Mwanza, Fatmah Kimwaga wakati wa semina iliyoratibiwa na taasisi hiyo kulenga kutoa elimu na kufanya majadiliano na walimu wakuu wa shule na watendaji wa kata wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ili kumaliza tatizo la mimba za utotoni, ndoa za utotoni na unyanyasaji wa kingono kwa watoto wa kike wilayani humo.

Alisema takwimu zinaonyesha mikoa ya Dodoma, Tabora na Shinyanga, imekuwa na ongezeko kubwa la mimba za utotoni huku wilaya ya Kishapu, ikiwa miongoni mwa wilaya zinazoongoza kwa tatizo hilo, hivyo ni lazima wazazi, walimu na watendaji wa kata washirikiane kutumia njia tofauti kuikabili changamoto hiyo.

Alisema walimu wanapaswa kujenga utaratibu wa vikao vya hadhara kuzungumuza na mabinti, vivo hivyo viongozi wa vijiji na kata nao wajitahidi kufanya majadiliano ya mara kwa mara na wazazi, kwani chanzo cha mimba za utotoni kipo sehemu zote kwa maana ya mashuleni na mitaani wanapoishi.

Alisema ingawa sheria zipo wazi juu ya watuhumiwa wa makosa ya mimba na ndoa za utotoni, bado kuna changamoto ya ucheleweshwaji wa hukumu, na kuliomba jeshi la polisi nchini kujitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati ili kuwabaini wote wanaohusika na mahakama iweze kuwachukulia hatua kwa mjibu wa sheria.

Mkufunzi wa Shule ya Sheria Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT)-Mwanza, Dk. Neema Mwita alitaja baadhi ya vyanzo vya ndoa na mimba za utotoni ni kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi, mawasiliano hafifu wakati wa balehe na mila na desturi hivyo aliwakumbusha viongozi kutumia sheria ya elimu, sheria ya mtoto ya 2009, sheria ya ndoa1979 na sheria ya kanuni za adhabu sura 16 ili kuwalinda watoto.

Ofisa Utumishi Wilaya ya Kishapu, Jovin Vedasto aliwashauri watendaji wa kata wanapopokea kesi zinazohusisha aina yeyote ya ukatili wa kijinsia kutohukumu kwa mazoea badala yake waripoti kituo cha polisi na dawati la jinsia kwa ajili ya upelelezi na pia wafanye kazi kwa ukweli na uwazi ili wasigeuke kikwazo cha up

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles