23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yajipanga kukabiliana na maafa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imesema itachukua hatua madhubuti za  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi  kwa kupunguza shughuli zote zinazosababisha madhara ambayo yanaweza kusababisha majanga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene Ofisini kwake Bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Msumbiji uliojadili kuhusu namna ya kuchukua tahadhari ya mapema katika hatua za kudhibiti Majanga.

Simbachawene alisema miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni pamoja na kuweka mifumo thabiti ya utayari kuhakikisha wananchi wanachama wanapata taarifa mapema pindi majanga yanapotokea na kudhibiti ukubwa wa madhara yake, na kuhakikisha makundi yaliyo katika hatari ya kuathirika na majanga wakiwemo Wanawake, Watoto na Watu Wenye Ulemavu wanafikiwa ili kuchukua hatua za tahadhari.

“Eneo lingine ni kuongeza uwekezaji  ili kuimairisha taasisi zinazohusika na  mifumo ya tahadhari za mapema na huduma za usimamizi wa maafa, kuimarisha mfumo wa kisheria wa kuziwezesha  mamlaka zenye dhamana ya tahadhari kama hapa kwetu ni Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), wanaokusanya taarifa na kuzipeleka na kushirikiana na vitengo vinavyohusika na majanga,”Alisema. Mhe. Simbachawene.

Aidha  amewahimiza wananchi kufuatilia taarifa za hali ya hewa zinazotelewa na wataalam  na kuzitumia katika shughuli za kila siku pamoja na watu wanaoishi katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa kuwa na mfumo wa kubadilishana taarifa na kusaidiana  kitaasisi  hatua itakayosadia kuepuka majanga kabla hayajatokea.

Ikumbukwe  Mkutano huo wa siku mbili ulifanyika Mjini Maputo nchini Msumbiji ulifunguliwa na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi kwa lengo la kupokea maoni ya maandalizi ya maafa na namna ya kushughulikia na kutekeleza maelekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress aliyezitaka nchi kuhakikisha raia wake wanapokea taarifa zinazoweza kusababisha majanga ikiwa ni mkakati wa kimataifa wa kupunguza madhara ya maafa ifikapo mwaka 2030.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles