27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

CHAVITA chaomba Serikali, wadau kuzingatia Wakalimani wa lugha

*ChahimizaWatanzania kuendelea kuchanja chanjo ya Uviko

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital 

Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) kimeomba Serikali, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuhakikisha vinazingatia kurishikisha wakalimani wa lugha ya alama ili kuwasaidia kipata elimu.

Mratibu wa wa masuala ya Jinsia kutoka CHAVITA ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya SHIVIWATA, Lupi Maswanya(kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Aidha, CHAVITA kimesema kuwa wakati wa janga la Uviko-19 kulikuwa na changamoto wa mawasiliano kwa watu wenye ulemavu wakati wa vipindi vilivyohusu uelimishaji wa janga hilo.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo Septemba 13, 2022 na Mratibu wa wa masuala ya Jinsia kutoka CHAVITA ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya SHIVIWATA, Lupi Maswanya.

“Katika kipindi cha janga la uviko-19 kulikuwa na changamoto kwa watu wenye ulemavu ambapo watu wenye ulemavu walikuwa hawapati elimu hata katika vipindi ambavyo vilikuwa vikielimisha kuhusu mlipuko huo kwani hakikuwa na mtafsiri wa lugha ya alama.

“Wito huu pia mbali na vyombo vya habari tunautoa kwa Serikali ambapo wamekuwa wakiacha nyuma wakalimani wa lugha ya alama kunapokuwa na mikutano ya kitaifa au warsha na makongamano mbalimbaki, hivyo tunaomba ilitazame hili ili kuleta jamii jumhishi,” amesema.

Amesema katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapatiwa chanjo ya uviko-19 hususan viziwi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) wanatekeleza mradi wa mwaka mmoja wa kutoa chanjo ya uviko kwa wilaya tatu za kila mkoa.

“Mikoa tuliyoanza nayo ni Arusha, Mbeya na Mwanza ambapo jumla ya watu waliochanja ni 42,961 lengo likiwa ni kufikia watu 51,000,” amesema.

Mwanasheria wa CHAVITA, Novath Rukwago(aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano huo.

Awali, Mwenyekiti  wa Shirikisho la Vyama vya walemavu Tanzania(SHIVYAWATA), Ernest Kimayo, amsema maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Viziwi Duniani amesema yanatarajiwa kufanyika mkoani Mtwara kuanzia Septe 25 hadi Oktoba mosi, mwaka huu yakiwa na kaulimbiu ya “Kujenga jamii jumhishi”.

“Katika maadhimisho haya mgeni rasmi tunatarajia atakuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa,” amesema Kimayo.

Upande wake, Mwanasheria wa CHAVITA, Novath Rukwago amesema kuwa pamoja na kutoa chanjo ya uviko kwa watu wenye ulemavu pia imekuwa ikihusisha watu wengine wasio na ulemavu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles