26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bingwa NMB Marathon kulamba miloni tatu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAKATI mbio za NMB Marathon zikitarajiwa kufanyika Septemba 24, imefahamika kuwa mshindi wa mbio hizo kwa kilomita 21 anatarajiwa kuondoka na kitita cha milioni tatu.

Hayo yalisemwa na Ofisa Mkuu Rasilimali Watu NMB, Emmanuel Akonai wakati akitangaza zawadi za washindi mbalimbali za marathon hizo ambazo huu ni msimu wake wapili kufanyika ambapo lengo lake ni kukusanya kiasi cha milioni 600 kwa ajili ya kuwakabidhi akinamama wenye ugonjwa wa fistula.

Afisa Mkuu Rasilimali Watu Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (wa pili kushoto), (NMB Chief of Human resources officer) akionesha zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa NMB Marathon 2022 jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitakazofanyika Septemba 24 zitaanzia na kuishia kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa NMB Marathon, David Marealle na kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa mbizo hizo, Suleiman Nyambui. (Na MPIGA PICHA WETU).

Mbio hizo zenye kauli mbiu ya Mwendo wa Upendo zinatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Leaders, Dar.

Akonai alisema: “Kwa mshindi wa kwanza kwa kilomita 21 kwa wanawake na wanaume watapata milioni tatu, wapili milioni 1.8, watatu laki nane, wanne laki sita, watano laki tatu na nusu, wasita laki mbili na nusu.

“Kwa upande wa kilomita 10, wakwanza milioni 1 kwa mwanamke na mwanaume, wapili laki nane, watatu laki tano, wanne laki tatu, watano laki mbili, wasita laki moja na nusu na kwa upande wa kilomita tano (kwa watoto) wa kwanza baiskeli yenye thamani ya laki sita, wapili vocha ya laki mbili na watatu smart watch ya laki mbili.

“Tunawaomba watu wote wenye nia njema waungane na sisi ili tuweze kufikia azma ya kutimiza kiasi hiki cha milioni 600,” alisema Akonai.

Kwa upande wake, Mratibu wa mbio hizo, David Marealle alisema: “Mwamko ni mkubwa kwa wale ambao wanaendelea kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki mbio hizi ambapo vituo vyetu vinaendelea kwa ajili ya kazi hiyo ya kuandikisha watu.

“Tutakuwa na siku tatu kwa ajili ya watu kuchukua vifaa zikiwemo namba na tsheti baada ya kujiandikisha ambazo ni Septemba 21, 22 na 23,” alimmaliza David.

Naye Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Riadha, Seleman Nyambui alisema: “Hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri kabisa na uzuri ni kuwa NMB Marathon kila mwaka kumekuwa na jambo lingine la tofauti ambalo wanakuja nalo.

“Mara nyingi ilizoeleka kuona washindi watatu wa juu pekee ndiyo ambao wanapewa zawadi lakini mara hii imekuwa tofauti kabisa na sisi tutahakikisha washindi wa haki wanapatikana kabisa, hakutakuwa na wale ambao watakatisha njia ili washinde,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles