24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yaahidi kusaidia Burundi kuingia SADC

Na Mwandishi wetu, Dar es Slaam

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kuisaidia Burundi ili ifanikiwe katika adhma yake ya kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kama ilivyoombwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, marehemu Pierre Nkurunziza wakati wa uhai wake.

Majaliwa  aliyasema hayo juzi alipozungumza kabla ya mazishi ya Rais Nkurunziza yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ingoma uliopo Gitega nchini Burundi.

,Majaliwa alisema ameshiriki mazishi hayo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

 “Marehemu Rais Pierre Nkurunziza alitamani sana kukabidhi madaraka huku akiwa ametimiza kiu yake ya Burundi kuwa mwanachama wa SADC jambo ambalo halikuwezekana, naamini Mheshimiwa Rais (Rais mteule wa Burundi Evariste Ndayishimiye) utalisimamia suala hilo hadi litimie”.

Alisema Rais Dk. Magufuli amemtuma afikishe salamu za pole kwa mke na familia ya marehemu, Rais wa Burundi  na wananchi wote kufuatia kifo cha Nkurunziza kilichotokea Juni 9, 2020.

Alisema Tanzania  na Burundi ni ndugu na anaamini undugu na mshikamano huo utaendelea kuwepo hata baada ya kifo cha Rais Nkurunziza ambaye alitoa mchango mkubwa katika kuuimarisha mshikamao  huo.

Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wa Burundi kumpa ushirikiano Rais wao mpya Ndayishimiye  kama walivyofanya  kwa marehemu  Nkurunziza.

Naye, Rais wa Burundi, Ndayishimiye alisema Serikali yake itayaenzi na kuyaendeleza mema yote yaliyofanywa na Marehemu Nkurunziza na aliwashukuru viongozi wote kutoka nje ya nchi yake ambao walishiriki katika mazishi hayo.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Rais Mstaafu  wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma Kikwete na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bujumbura juzi asubuhi Juni 26, 2020, Majaliwa alipokelewa na Waziri Mkuu wa Burundi, Prosper Bazombaza.

Baada ya mazishi hayo Majaliwa alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Burundi  kabla ya kurejea nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles