27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watakiwa kujiepusha na migogoro ili kupunguza kesi mahakamani

Na SHEILA KATIKULA- MWANZA

WANANCHI wa Mkoa wa Mwanza, wameombwa kujiepusha na migogoro mbalimbali ili kupunguza kesi zilizopo mahakamani.

Wito ulitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya  Uhuru, Dk Derick Nyasebwa kwenye sherehe za kuhitimisha mafunzo ya awali kwa wahitimu 68 ya uangalizi wa jamii yaliyoandaliwa na Shirika la Mfumo na Muundo wa Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA).

Dk Nyasebwa alisema wapo baadhi ya watu hufanya migogoro kuwa chanzo cha kujipatia kipato.

 Alisema migogoro husababisha kukosa amani na furaha  na husababisha magonjwa hivyo ni vema katika maisha kujiepusha  nayo.

Alisema katika baadhi ya nchi zenye migogoro mikubwa huita wajumbe kutoka sehemu mbalimbali ili waweze kusuluhisha kesi zao.

“Binafsi sipendi migogoro iwepo sehemu yoyote, ila wapo baadhi ya watu wamefanya (migogoro) kama sehemu ya maisha yao, pindi wanapokuwa na kesi  wakisuluhishwa hawataki kufikia mwafaka kwa sababu hujipatia fedha kwa kazi hiyo na kuifanya kuwa sehemu ya kitega uchumi,”alisema Nyasebwa.

Naye Mwanasheria wa Kujitegemea, Remigius Mainde alisema lengo la Mujata ni kutokomeza uhalifu, kuelimisha jamii ili waweze kufanya mambo mema na  kupunguza kesi zilizopo mahakamani  za uhalifu.

Alisema ni vema vijana kutimiza malengo ya  Mujata kwa kufanya majukumu yao waliyofundishwa ili kupunguza vitendo vya  uhalifu na waweze kusaidia kundi hilo na kutoka katika mazingira ya uhalifu ili  jamii iwe sehemu salama na kujiepusha na kupokea rushwa.

“Watimize malengo  yao na wajiepushe na vitendo vya rushwa pindi watakaposhawishiwa kwani vijana huingia kwenye makundi hatalishi na kufanya uhalifu na kuvunja amani,”alisema Mainde.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa  shirika hilo, Jacob Matiko, alisema waliamua kuanzisha mafunzo hayo kanda ya ziwa baada kuona changamoto nyingi zinawakabili vijana kwani wapo watu huwashawishi  vijana hao na kufanya uhalifu  kupelekea kuvuanja  wa amani.

Mwenyekiti wa Bavicha  Mkoa wa Mwanza, Boniphace Nkobe, aliwataka vijana hao kutumia mafunzo yao vyema  kwa kufichua watu ambao wanawaficha watoto  wenye walemavu ndani na kukosa haki zao za msingi.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu, Ayub Michael alishukru shirika hilo kwa kuandaa mafunzo hayo ya miezi mwili ambayo atasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles