24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania sasa kivutio cha uwekezaji-Balozi Marekani

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Balozi wa Marekani nchini, Dk, Donad Wright amesema kwasasa kuna sera zinazoifanya Zanzibar na Tanzania kuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutoka nchini kwake.

Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright akitaka utepe kuzindua ofisi za Kampuni ya Re/Max Costal zilizopo barabara ya Chole Oysterbay, Dar es Salaam jana ambayo inajishughulisha na biashara ya ukodishaji na mauzo ya mali zisizohamishika pamoja na kupangisha.

Dk. Wright ambaye yupo nchini kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, aliyasema hayo juzi wakati akizindua ofisi ya Dar es Salaam ya kampuni ya uuzaji na ukodishaji wa majengo ya Re/Max ambayo asili ni Marekani.

Amesema tangu alipoteuliwa kuiwakilisha nchi yake hapa nchini, kipaumbele chake kimekuwa ni kukuza urari wa biashara baina ya Tanzania na Marekani na mwaka huu nchi hizo zinasherehekea miaka 60 ya ushirikiano.

“Hivi karibuni nilifarijika kusikia Serikali ya Zanzibar na imetangaza mpango unaowaruhusu wawekezaji wa kigeni kuchukua fursa za unafuu wa kodi na vibali vya makazi visiwani humo.

“Sera za namna hiyo zinaendelea kuifanya Tanzania na Zanzibar kuwa kivutio zaidi cha wawekezaji wa Kimarekani,” amesema Balozi huyo.

Mmiliki wa Kampuni ya Re/Max Costal, Stephi Hill Said(katikati),akiwaonyesha nembo ya kampuni hiyo, Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright (kulia), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Simai Mohammed Said na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali wakati wa uzinduzi waa ofisi zaa kampuni hiyo zilizopo mtaa wa Chole Oysterbay, Dar es Salaam.

Upande wake, Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Jamal Kassim ambaye alikuwa sehemu ya walioshuudi ufunguzi wa ofisi hiyo amesema hivi aribuni Zanzibar imepitisha sera ambayo ni kivutio kikubwa cha uwekezaji  katika sekta ya makazi  visiwani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles