23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kuwa kitovu cha usambazaji dawa za binadamu Afrika

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Uwepo wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767- 300F ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) imeichochea Kampuni ya utengenezaji dawa za binadamu ya Glenmark Pharmaceutical ya nchini India kukubali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usambazaji wa dawa barani Afrika kwa kutumia ndege hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.

Hayo ameyasema Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ziara ya kikazi aliyoifanya jijini Mumbai, India ambapo alifanikiwa kukutana na wadau mbalimbali zikiwamo kampuni kubwa za uzalishaji na usambazaji wa dawa.

“Katika ziara hiyo tulifanikiwa kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo kampuni kubwa ya uzalishaji na usambazaji wa dawa, kampuni uuzaji wa tiketi, kampuni kubwa za Ndege, uongozi wa hospitali mbili kubwa jijini Mumbai.

“Hii ni tangu utoaji wa huduma, kununua ndege mpya za kisasa na kupanua mtandao wa safari ili kuendana na kasi ya mahitaji halisi ya soko la anga. Kwa sasa tuna ndege mpya masafa ya mbali tatu – Boeing 787-8 mbili na Boeing 767-300F moja, masafa ya kati nne – Airbus 220-300 na masafa mafupi sita – Q400.

“Tangu kuanza kwa utekelezaji wa Mpango Mkakati wetu, tumeendelea kuboresha huduma kama mnavyofahamu, India ni soko jipya la utalii kwa Tanzania na sisi ATCL tunalipa umuhimu wa pekee soko hilo kutokana na fursa zilizopo katika soko hilo,” amesema Mhandisi Matindi na kuongeza kuwa soko hilo linakadiriwa kuwa na watu bilioni 1.4.

Amesema kwa kutumia ndege za abiria walifanikiwa kumiliki asilimia 80 ya abiria wote wanaosafiri kati ya Tanzania na Mumbai sawa na wastani wa abiria zaidi ya 66,000 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles