24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

WANTS: Tunataka wasanii watambulishwe na kazi zao siyo vituko

*Kuja na Tamasha la Wasanii Wanawake Tanzania Novemba 23 hadi 25

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ukosefu wa elimu inayohusu namna ya kutambua haki zao ni moja ya sababu iliyotajwa kama kikwazo cha kukwamisha wananwake wengi nchini kuingia katika sanaa huku hawa wale wachache waliopo nao wakikabiliwa na changamoto hiyo.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Mtandao wa Wasanii Wanawake Tanzania(WANTS), Agnes Lukanga wakati akizungumza na Mtanzania Digital kuhusu hali ya tasnia hiyo nchini hususan kwa wanawake ikiwa ni miezi michache imesalia kabla ya Tamasha la Wasanii Wanawake Tanzania linalotarajiwa kufanyika Novemba 23 hadi 25, mwaka huu Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Agnes anasema kuwa vipaji vingi vya wasanii wanawake vinashindwa kuonekana na wakati mwingine kupotea kabisa kutokana na changamoto lukuki zinazowakabili.

“Wasanii wengi wanachukuliwa kufanya sanaa bila kuwa na ufahamu juu ya haki zao na stahiki wanazotakiwa kuzipata baada ya kuwa wamefanya kazi, hivyo sisi Mtandao wa Wasanii Wanawake Tanzania(WANTS) kwa kushirikiana na wadau kama COSOTA tunaendelea kutoa elimu kwa wasanii wanawake.

“Kuna wadau wengine kama Women Fund Tanzania na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) wamekuwa wakisaidia kuwezesha utoaji wa elimu kwa wasanii wanawake,” anasema Agnes na kuongeza kuwa:

“Mwamko umekuwa ni mkubwa sana sana katika kihakikisha kuwa wanawake wanasimama, mfano wakati wa janga la Uviko 19 mafunzo haya yaliwasaidia sana wanawake kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri kwenye kuwapa elimu ya Tehama.

“Sasahivi tunaona wanawake wengi wanajitokeza kujua haki zao, mfano wengi waliokuwa wakitumika kingono ili wapewe nafasi ya kuigiza au kufanya sanaa wamekuwa wakija na kutwambia kuwa kuna jambo hili na lile, lengo nikihakikisha kuwa maneno haya yanaondoka kabisa,” anasema Agnes.

Anasema wanaimani kuwa elimu ikiwafikia walio wengi basi vitendo hivyo vitaisha kwenye jamii na wasanii wanawake watafanya kazi zao bila bughudha.

“Tunataka wanawake wanaofanya sanaa watambue na kujua haki zao, kwani tunataka ifikie chini kwenye ngazi za kanda, wilaya, mkoa na hatimaye taifa. Hatutaki kuanza na wasanii mahiri lakini tunataka hata hawa wadogo wahakikishe kuwa wanafanya vizuri.

“Naiona sanaa ya Tanzania mwanamke akiwa huru bila vikwazo, pili tumewekewa mfuko wa sanaa na utamaduni katika kuhakikisha kuwa wanawake wasanii wanapata kipato kupitia kazi zao,” anasema Agnes.

Anaongeza kuwa wanaamini kuwa miaka michache ijayo Tanzania itakuwa na wasanii imara ambao watakuwa na uwezo wa kujisimamia, kwani kupitia tamasha hilo wanatarajia makubwa kuanzia eneo la bajeti kwani litashirikisha watunga sera na wadau wengine.

“Vitendo vya unyanyasaji vimekuwa moja ya sababu kubwa ya wazazi kutokuruhusu wanawake kufanya sanaa. Unajua maeneo mengi ya kufanyia sanaa ni hafifu mfano mazozi mengi yanafanyika baa ambayo kiujumla ni kama hayatoa hadhi ya sanaa, watu wanakuja kumtambua mtu akiwa juu lakini huko chini mazingira yake hakuna hata mmoja anayemsapoti”

“Sanaa ni kazi na inahitaji umakini, nidhamu na adabu bila kusahau kujitambua kwamba wewe ni nani unataka kwenda wapi, tusiiangalie sanaa kama ngazi ya mtu kufika sehemu flani bali pia iangaliwe namna ya kuwekewa misingi stahiki na yenye hadhi ili kesho wawe walipakodi wa nchi.

“Wazazi wana nafasi kubwa ya kufanya watoto wa kike waingie kwenye sanaa na kushiriki kikamilifu ikiwamo kuboresha mazingira ya sanaa. Kwani sanaa siyo uhuni wala siyo sehemu ya watu waliokosa chakufanya kukimbilia, ndiyo sababu tunapata watu ambao badala ya kutambulishwa na kazi zao wanatambulishwa na vituko kwa lengo la kujulikana jambo ambalo ni makosa makubwa,”

Agnes Lukanga.

“Wazazi wana nafasi kubwa ya kufanya watoto wa kike waingie kwenye sanaa na kushiriki kikamilifu ikiwamo kuboresha mazingira ya sanaa. Kwani sanaa siyo uhuni wala siyo sehemu ya watu waliokosa chakufanya kukimbilia, ndiyo sababu tunapata watu ambao badala ya kutambulishwa na kazi zao wanatambulishwa na vituko kwa lengo la kujulikana jambo ambalo ni makosa makubwa. Wenye nidhamu wamewekwa kando ili kupisha wanaojianika kuwa maarufu.

Tamasha la wasanii wanawake linatarajiwa kufanyika makumbusho ya taifa kuanzia Novemba 23 hadi 25, mwaka huu likiwa na kaulimbiu inayosema Sanaa ni Uchumo, ondoa vikwazo kwa wasanii wanawake ili kukuza pato la taifa”,” amesema Agnes.

Upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania, Cynthia Henjewele anasema kwa sasa Serikali iko karibu na wasanii na kwamba wanamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatika Waziri mchapakazi Balozi Dk. Pindi Chana.

“Tushukuru Serikali kuwa karibu na wasanii na wakina mama, tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupa jembe letu Waziri Balozi Dk. Pindi Chana kwani tuko naye bega kwa bega, tumeona COSOTA mirabaha wasanii wanapata Bakita pia tunavyoshirikiana nao.

“Sasahivi tumejiunga na Basata na bodi ya filamu hivyo tuko katikati. Pamoja na hayo niwakumbushe baadhi ya viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kupendelea wasanii huku wengne wakiachwa jambo ambalo halina afya kwa sanaa yetu.

“Tumeona mama yuko bega kwa bega kusaidia sanaa yetu, mama anataka tuishi kama tuko Hollywood hivyo kina mama mpambane, washikeni mkono akina mama ambao hawana ofisi. wajitahidi kutetea wasanii. Pamoja na hayo tusiache maadili tuangalie vijana wetu wakoje, ndoa za jinsia moja hii mambo ya ushoga tusochoke kukemea ushoga…tunaona kwasasa hali inaanza kuwa nzuri. Hivyo tusichokeee,” amesema,” amesema Cynthia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles