22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkumbo azindua kitabu cha Kijana wa Tofauti, awakumbusha vijana kujipambania

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema vijana wengi nchini wanakabiliwa na changamoto ya kushindwa kujipambania badala yake wanataka kupambaniwa katika mambo mbalimbali kwasababu ya ubinafsi na ushindani.

Prof. Mkumbo amebainisha hayo Agosti 12, jijini Dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha “Kijana wa Tofauti” kilichoandikwa na Mtanzania, Amani Sanga, ambapo amewasisistiza vijana kupambana kwa uwezo wao na siyo kusubiri kubebwa.

“Vijani wengi wanataka kupambaniwa katika mambo mbalimbali mfano katika ajira mtu kasoma kafaulu vizuri lakini kwenye ajira anataka kupambaniwa pambana kwa uwezo wako na bidii yako,” amesema Prof. Mkumbo.

Amesema vijana wanapaswa kuangalia tafsiri ya maendeleo yao nakwamba watu wengi wanatamani mafanikio ya watu wenginebadala ya kutengeneza talanta ambayo ndiyo hatua ya kwanza.

Amesema vijana kutokuwa na hali ya kutafuta maarifa, kuthamini maarifa, ujuzi, bidii katika kazi na chanzo cha maarifa ni moja ya changamoto inayowakwamisha wengi.

Aidha, Prof. Mkumbo amewasisitiza vijana kuwa na maadili na uaminifu pindi wanapopata kazi katika sekta mbalimbali nchini wasiwe na tamaa.

“Tunatarajia kuaandaa dira ya maendeleo ya mwaka 2050, mchakato huo utatengeneza fursa za uchumi na tutahakikisha katika timu vijana wanakuwepo.

Naibu Balozi wa Kudum Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York, Dk Sulemani Haji Suleiman.

Upande wake Balozi Naibu wa Kudumu Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York, nchini Marekani, Dk. Suleiman Haji Suleiman amesema namba ya Watanzania walioajiriwa katika Umoja wa Mataifa bado ni ndogo.

“Kuna fursa nyingi kwenye Umoja wa Mataifa ya kuongeza vijana kwenye ajira lengo ni kumkomboa kijana kiuchumi miradi iliyoanzishwa na kupanua wigo wa maendeleo ikiwamo kuwekeza katika biashara, utalii, kilimo na mengine,” amesema Dk. Suleiman.

Naye Mwenyekiti wa Glob Youth Empowerment Institute, Edger Gasper amesema hiyo ni jumuiya ya vijana kutoka sehemu tofauti na zaidi vijana 400 walihudhuria uzinduzi huo na uliofanyika siku ya vijana duniani.

“Vijana wanakabiliwa na changamoto ya ajira, lazima ufikirie nje ya boksi kuweza kuwasaidia katika hili,” amesema Gasper.

Mwenyekiti wa Glob Youth Empowerment Institute, Edger Gasper.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Glob Youth Empowerment Istitute na Mwandishi wa Kitabu ‘Kijana wa Tofauti’, Amina Sanga amesema kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha tatu za Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa huku pia kikizingatia lugha ya alama ili kila mmoja aweze kusoma.

“Hiki ni kitabu changu cha tisa na mizingatia hata kwa watu wasiopenda kusoma basi watasikiliza kwa njia ya sauti, naamini kupitia vitabu vyangu vijana wataleta mabadiliko katika jamii na tunatarajia kuwafikia vijani walioko vijijini na kuwapa elimu za kujiajiri na kutafuta fursa hiyvo leo tunamsherekea kijana wa tofauti,” amesema Amina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles