27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

NIC yatunukiwa tuzo ya Superbrand, yaahidi huduma bora

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Bima la Taifa(NIC) limepokea tuzo na cheti kutoka Kampuni ya Superbrand ikiwa ni matokeo ya kazi wanazofanya katika kuhudumia wananchi na ubora wa utoaji bidhaa.

Akizungumza Agosti 14, jijini Dar es Salaam baada ya kupokea tuzo na cheti Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dk. Elirehema Doriye amesema wataendelea kuja na ubunifu wa bidhaa ambazo zitagusa watu wote.

Amesema cheti hicho cha Superbrand kinaonyesha ubora wa huduma zinzotolewa na Shirika hilo na namna mteja anavyoridhika na huduma zinazotolewa.

“Leo ni siku ya kipekee kwetu kama shirika kwani ni mara ya kwanza kupokea cheti/tuzo hii ya superbrand, hii inaonyesha namna tunavyofanya kazi vizuri katika kuwahudumia wananchi kwetu huu ni mwanzo tutaendeleza kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania,” amesema Dk. Doriye.

Amesema ongeza kuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni inayomilikiwa na Serikali kupata cheti hicho na kwamba hayo ni mafanikio kwa Serikali na taifa kwa ujumla.

“Hii inaonyesha ni mafanikio makubwa kwa Serikali kwani hayo ni maono na maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu ndio yaliyopelekea kufikia mafanikio haya ambayo leo ndiyo tumeona matokeo yake,” ameongeza.

Amesema kufuatia utafiti huru uliofanywa na Kampuni ya Superbrand wa kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ndio umetoa mwanga wa namna bima hiyo inavyofanya kazi na kuwatofautisha na kampuni nyingine za bima.

Aidha, Dk. Doriye amesema wanatarajia kuboresha zaidi matumizi ya teknolojia ili kuwafikia wananchi kila sehemu na kuendelea kutoa elimu zaidi.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Superbrand Afrika, Jawad Jaffer amesema upatikanaji wa tuzo hiyo kwa NIC walifuata vigezo ikiwemo kufanya utafiti kwa nchi za Afrika Mashariki.

Amesema wameweza kuwafikia wananchi katika nchi hizo na kuwauliza kuhusu huduma za bima wanazotumia na kuona watu wengi kuvutiwa zaidi na huduma zinazotolewa na NIC.

“Ili kutoa hiki cheti cha Superbrand kwa taasisi na mashirika tunafanya utafiti wa kutosha ikiwemo utoaji wa huduma na ubora wa bidhaa kwa watumiaji katika sekta ya bima utafiti ulionyesha watu wengi kuvutiwa na huduma zinazotolewa na shirika hilo,” amesema Jaffer.

Kampuni ya Superbrand imetoa tuzo kwa taasisi za umma na sekta binafsi tano ambazo ni Shirika la Taifa la bima(NIC), Banki ya NMB, Kampuni ya GSM, kampuni ya Bonite Bottles kupitia maji yake ya Kilimanjaro na Dar Caramica Center.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles