29.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kushiriki kombe la dunia -Mchengerwa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania inatarajia kushiriki kwenye mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kumalizika mashindano ya mwaka huu 2022 yanayofanyika Qatar kutokana na mikakati kabambe ya maandalizi inayoendelea hivi sasa.

Mchengerwa amesema hayo leo Februari 8, 2022 jijini Dar es Salaam kwenye halfa iliyoandaliwa na ubalozi wa Qatar, kuadhimisha siku ya michezo ya nchi hiyo inayofanyika kila jumanne ya mwezi Februari kila mwaka, ambapo Balozi Hussain bin Ahmad Al Homaid na Waziri Mchengerwa waliongoza mazoezi ya kutembea uwanjani  kama ishara ya ushiriki wa maadhimisho ya siku hiyo.

Katika halfa hiyo aliyoambatana na Katibu Mkuu wake, Dk. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, amesema Tanzania inakusudia kushiriki katika mashindano hayo kutokana na mikakati kabambe iliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya michezo nchi nzima.

“Sisi kama taifa ni muhimu tukubali ili kufanikisha zoezi hili la kushiriki  mashindano makubwa kama haya  lazima kujiandaa  na kuboresha  miundo mbinu ya michezo ambapo  kwa sasa  tumeshatenga shule 56 nchi nzima  kwa ajili ya michezo,” amefafanua Mchengerwa.

Aidha, amesema Serikali inakusudia kujenga viwanja vikubwa vya ndani ambavyo vinajumuisha michezo mbalimbali viwili kwenye mji wa Dar es Salaam na Dodoma pia tunatarajia kujenga maeneo makubwa ya burudani.

Amemwomba Balozi wa Qatar, Hussain Bin Ahmad Al Homaid kuisaidia Tanzania kwenye eneo la miundombinu ili kuendelea kuimarisha uhusiano uliojengeka baina ya nchi hizo mbili.

Amemhakikishia Balozi kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ipo tayari kuendelea kushirikiana wakati wowote kwenye sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni kwa faida ya wananchi wa nchi zote mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles