23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia kuweka jiwe la msingi mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan kesho (Februari 9,2022) anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje (Outer Ring Road) katika Jiji la Dodoma yenye urefu wa Kilomita 112.3.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Februari 8,2022 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ofisini kwake jijini hapa katika kikao chake na waandishi wa habari na kuongeza kuwa barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami hali itakayoruhusu uwepo wa fursa mbalimbali.

Amesema hafla ya uwekaji jiwe la msingi itafanyika katika eneo la Makutupora-Veyula kuanzia saa 1:00 asubuhi ambapo maandalizi yote muhimu yamekamilika.

Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amefafanua kuwa ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 221 na kwamba ujenzi huo utakamilika ifikapo mwaka 2025 na kuweka mandhari safi ya Jiji la Dodoma.

Akitaja fursa zitakazo tokana na barabara hiyo,Mtaka amesema itakuwa kiungo muhimu kwa barabara nyingine za Jiji la Dodoma ikiwa imegawanywa kwa wakandarasi wawili ambao ni M/sAVIC INTL Project na China Civil Engineering Construction Cooperation zote kutoka Jamhuri ya watu wa China.

Mtaka pia ametumia nafasi hiyo kuzitaka taasisi zote za Serikali mkoani hapa,taasisi binafsi,makundi mbalimbali na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika hafla hiyo ili kubaini mapema fursa nyingi zitakazo patikana kupitia ujenzi huo.

“Kwa kuwa wananchi Wana fursa nzuri ya kushiriki,Mtaka amelielekeza jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma kuruhusu madereva wa daladala (kukatisha ruti) kufanya usafirishaji wa abiria kutoka sehemu mbalimbali ili kurahisisha huduma hiyo ili watu waweze kufika kwa wakati katika eneo hilo,”amesema Mtaka.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara nchini(TANROADS)Mkoa wa Dodoma Injinia Leonard Chimagu amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ya mzunguko utajengwa kwa awamu mbili .

Amefafanua kuwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa Kilomita 52.3 kupitia Nala,Veyula,Mtumba na Ihumwa wakati awamu ya pili itahusisha Kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu na Nala.

Injinia Chimagu amesema ujenzi huo ukikamilika utafungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Dodoma ikiwa ni pamoja na kuondoa msongamano wa magari uliopo sasa kwa kuwa magari yanayoenda mikoa mingine watatumia barabara hizo bila kupitia ndani ya Jiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles