28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kuja na mwarobaini wa masoko ya mazao ya chakula

*Teknolojia nayo yatajwa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amekiri kuwa ni kweli suala la masoko bado ni changamoto lakini katika tafiti walizofanya wamegundua kuna mambo mawili yenye utata na wanafanyia kazi.

Hayo amezungumza leo Septemba 7, jijini Dar es Salaam Dk. Samia alipokuwa akijibu swali kutoka kwa kijana aliyehudhuria Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF) uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Julius Nyerere (JNICC).

Swali hilo lilikuwa ni kwa namna gani Serikali ya Tanzania inatatua changamoto na kuhamasisha upatikanaji wa masoko na uongezaji thamani kwa bidhaa zinazozalishwa na vijana.

Ametaja changamoto hizo kwanza ni food balance sheet requirements bidhaa gani inatakiwa wapi ndani na nje ya nchi wakijua hilo watakua wanajua kitu gani wazalishe kiende upande mwingine.

“Pili ni connection ya mkulima na soko na lenyewe hatujaifanya kazi vizuri bado tumeanza kufanya kwenye baadhi ya mazao mfano korosho na tumeshuhudia mara kadhaa bei ya korosho ikipanda kwa sababu tunaunganisha ushirika wa mkulima na mnunuaji moja kwa moja tunamuondosha mtu wa kati baadhi wanakwenda moja kwa moja kwa mkulima kumeleta matokeochanya,” amesema Dk. Samia.

Amesema kwasasa wanunuzi wananunua korosho kutoka kwenye vyama vya ushirika vya wakulima hivyo wakulima wanapata fursa ya kushindanisha bei, jambo ambalo limepelekea bidhaa hiyo kupanda bei pia ameitaja bidhaa ya mbaazi pia ikiwa moja ya bidhaa ambazo zimefanikiwa kupata soko zuri kutokana na jitihada hizo.

Amesema jitihada zingine zinazochukuliwa na Serikali ni kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa kujenga barabara zinazounganisha mkoa mmoja na mwingine pamoja na wilaya zake na barabara kuu na nchi za jirani ili kuyafikia masoko ya nchi jirani kwa kusaidia mazao kutolewa shambani.

Ameongeza kuwa jitihada hizo zinakwenda sambamba na kuboresha bandari zilizopo nchini akiitaja bandari ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga na Mtwara.

Amesema Serikali inajenga eneo maalumu la kuhifadhi mazao yanayoharibika kwa haraka ili wakati yanasubiri usafiri wa meli yaweze kupata hifadhi.

Aidha amesema Serikali imenunua ndege ya mizigo iweze kusafirisha mazao yanayoharibika kwa haraka [Hotculture] kwani ndege hiyo itasafirisha mazao na kuyapeleka nje jambo ambalo litaepusha kutumia usafiri wa jirani ambao unaweza kuwa na changamoto nyingi ikiwemo za kubadilisha umilika wa bidhaa hizo.

Amesema kuwa Serikali inasaidia kutafuta na waongeza thamani kwa mazao ambayo yamepatikana ili yanapoingia sokoni yawe na ubora.

Dk. Samia amesema Tanzania inakubaliana kwenye karne ya ICT kutumia Teknolojia ya kisasa kwa sababu haikwepeki na teknolojia kurahisisha kilimo kwa vijana.

Amesema asilimia kubwa ya wengi ni vijana hivyoo ametoa fursa kwa kusikiliza na kuwa na majadiliano na vijana kujadili changamoto zinazowakabili kwenye biashara ya kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles