27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Samia: Ni aibu Afrika kulalamika juu ya ukosefu wa chakula

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema asilimia 65 ya ardhi barani Afrika inafaa kwa kilimo hivyo ni aibu kwa nchi za Afrika kuwa walalamikaji juu ya ukosefu wa chakula wakati ardhi ipo ya kutosha.

Dk. Samia ametoa kauli hiyo leo Septemba 7, jijini Dar es Salaam wakati akihutubia Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) mbele ya marais kutoka nchi mbalimbali kujadili juu ya nini kifanyike kuboresha mifumo ya chakula Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.

Amesema Jukwaa hilo la AGRFlinatumika kutoka na suluhu ya changamoto ya chakula na kwamba viongozi wa Afrika wapo tayari.

“Asilimia 60 ni vijana ambao nguvu kazi ya sisi viongozi wa Afrika tupo tayari kuondoa aibu ya Afrika kuwa walalamikaji, tupo tayari kulisha Afrika na duniani kwa ujumla,” amesema Dk. Samia.

Amesema licha ya rasilimali zilizopo Afrika wamebaki kuwa walalamikaji baada ya kutafuta suluhisho kuelekea njia ya mapinduzi ya uchumi wa kijani.

” Tupo na AGRF washiriki wa maendeleo sekta binafsi wasomi na wataalamu kubadilisha uzoefu namna ya mnyororo wa thamani ya bidhaa za kilimo na kujadili mipango ya kuimarisha usalama wa chakula Afrika,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema ili kufikia malengo viongozi wa Afrika hawana budi kufanya tathmini ya vipaombele vyao wavioanisha na mahitaji sasa katika muktadha wa dunia.

Amesema zaidi ya watu milioni 283 wanalala njaa barani Afrika hivyo ni wakati wa viongozi wa bara hilo kufanya tathimini.

Naye Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto amesema ardhi ya kilimo ipo Afrika na mkutano huo wa AGRF ni somo kubwa na hawawezi kuishi bila chakula, teknolojia na muda kwa sababu vitu hivyo ni muhimu.

“Tunaweza kuchochea biashara ya kilimo kuacha kuwa watu wa kulalamika wakati ardhi tunayo ni suala la kuongeza uzalishaji na tunafanya je? wakulima wazalishe zaidi,” amesema Rais Ruto.

Amesema katika somo la mkutano huo wa AGRF ni jinsi gani watafanya nini kubadilisha wakulima wazalishe kwa wingi na gharama za vyakula zipungue.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles