22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mr Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albamu mpya

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

STAA wa muziki, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala la kuachia rekodi tamu yenye burudani ya kipekee kwa jamii na sasa ameachia kitu kipya.

“Advice,” ni kazi mpya kutoka staa huyo ambayo imetiwa mkono na lebo maarufu nchini Ghana, M.O.G. Beatz, ikiwa inapatikana katika albamu inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’, itakayotoka rasmi Oktoba 27, mwaka huu.

Advice unawataja baadhi ya watu mashuhuri ulimwenguni wakiwemo Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila na Ken Saro-Wiwa, mwandishi na mwanaharakati wa Nigeria ambaye mwaka 1995 alichomoza zaidi ndani na nje ya nchi ya Nigeria.

“Nilikuwa nikitoka mahali pa kuwa na nguvu hiyo,” Mr. Eazi anasema.

Katika albamu hiyo ambayo ina ngoma 16, staa wa muziki nchini Kenya, Alphonce Odhiambo maarufu kama Alpha ODH, ameshirikishwa.

Mr. Eazi alichagua mwenyewe wasanii 13, wanaowakilisha nchi nane za Afrika, akiwaalika kushirikiana katika mchakato anaoutaja kuwa ‘usio rasmi na wa silika’.

“Kualika wasanii kwa ajili ya albamu hii kulitokana na shauku yangu ya ubunifu na kujitanua zaidi katika nchi zetu za Kiafrika. Kazi za sanaa hufungua mawazo, hisia, na nishati ndani ya muziki wangu,” anasema Eazi.

Kazi za sanaa iliyoundwa kwa ajili ya albamu hiyo zitaonyeshwa katika maonyesho ya hisia nyingi, ambayo yataanza kutumika Accra, Ghana.

Ni albamu iliyorekodiwa katika kipindi cha miaka miwili katika maeneo mbalimbali kama Ouidah na Cotonou, Benin; Kigali, Rwanda; Accra na Kokrobite, Ghana; Lagos, Nigeria; London; Los Angeles; na New York City, Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles