23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania iko tayari kwa wawekezaji kutoka Kenya- Rais Samia

Nairobi, Kenya

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema nchi yake iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya.

Samia ambaye amewahutubia wafanyibiashara kutoka Kenya na Tanzania amesema hakuna nchi inayoweza kunawiri pekee yake bila ushirikiano.

Rais huyo anayekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Kenya amesema serikali yake imechukua hatua ya kuleta mageuzi ili kufanya mazingira ya kufanya biashara kuwavutia wawekezaji kutoka Kenya kwa lengo la kutumia fursa zilizopo.

Samia

Samia amesema Tanzania ina ardhi, vivutio vya utalii na raslimali ambazo zinaweza kutumiwa kuboresha hali ya kiuchumi wa mataifa yote mawili. Ameongeza kwamba sekta ya kibinafisi ni nguzo muhimu sana ya kuhakikisha kwamba nafasi za ajira zipo kwa wananchi wa mataifa yote.

Aidha, miongoni mwa masuala ambayo Rais Samia amesema serikali yake inayashughulikia ili kufanikisha biashara nchini Tanzania ni pamoja na;

 • Kuhakikisha kwamba mazingira ya kibiashara yanaboreshwa
 • Mfumo mwafaka wa kodi unatumika nchini Tanzania
 • Sheria na sera za kuwavutia wafanyibiara
 • Mfumo mwafaka wa mahakama
 • Hali nzuri ya kuvutia uwekezaji

Mageuzi ya kufanikisha biashara

Rais Samia amesema Tanzania kwa sasa imetekeleza mageuzi yafuatayo ili kuhakikisha kwamba biashara zinanawiri nchini mwaeke ;

 • Inatathmini upya kodi na vikwazo visiyo vya kodi
 • Kurahisisha utoaji wa vibali vya kufanya kazi kwa wawekezaji wa kigeni
 • Kutathmini kodi na ada zinazotozwa biashara na watu
 • Usimamizi mzuri wa mfumo wa kodi
 • Kuimarisha vita dhidi ya ufisadi hasa katika sekta ya utumishi wa umma
 • Kufanikisha oparesheni za afisi ya pamoja ya kushughulikia biashara na uwekezaji
 • Kupeana ardhi ya kutumiwa kwa uwekezaji

Rais Samia ameongeza kwamba lengo lake ni kuhakikisha kwamba Wawekezaji wa kigni wanajenga imani ya kuwekeza nchini Tanzania na ili kurahisisha hilo serikali imeanzisha miradi mbali mbali ya kimkakati ikiwemo ya moiundo mbinu kama barabara,reli , bandari na kawi ili kupunguza gharama ya kufanya biashara .

Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema nchi zote mbili zitachukua hatua ya kuhakikisha kwamba makubaliano yote yaliyoafikiwa na mawaziri wa Biashara wa nchi zote yanatekelezwa.

Kenyatta ameongeza kwamba mwaziri hao watakutana katika kipindi cha wiki nne zijazo ili kujadili kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya kodi ambavyo vinaathiri biashara kati ya Kenya na Tanzania .

Akimalizia hotuba yake Samia aliwachekesha washiriki katika mkutano huo kwa kusema kwamba wawekezaji hawafai kushindwa kuwekeza nchini Tanzania aliposema;

“Mna bahati kwamba nchi zetu mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na.. upande mwingine kuna Suluhu ya kuondosha vikwazo vya biashara,” amesema Samia.’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles