Tanga Cement yajitosa mapambano dhidi ya corona

0
694

Amina Omari, Tanga

Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Tanga (Tanga Cement), kimekabidhi msaada vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa corona wenye thamani ya Sh milioni 20.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella, Mtendaji Mkazi wa kiwanda hicho, Mhandisi Benedict Lema amesema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Bombo na Jeshi la polisi.

“Msaada huu ni kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, hivyo sisi kama kiwanda tumeguswa kusaidia,” amesema Mhandisi Lema.

Kwa upande wake Shigella amewataka wawekezaji wengine kuacha kubweteka kwa sababu ya janga la corona bali waendelee na uzalishaji kama ambavyo serikali imeelekeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here