30.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Tanesco yaja na WhatsApp kwa wateja wote nchini

Bakari Kimwanga, ARUSHA

SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limeweka mfumo maalumu wa kutumia makundi ya WhatsApp kwa lengo la kutoa na pokea taarifa za nishati ya umeme kwa wateja wao wa kada mbalimbali nchini.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili jana Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco,  Leila Muhaji  alisema kuanzishwa  huko kwa makundi ya WhatsApp ni agizo kutoka bodi ya shirika hilo mkakati ukiwa ni kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.

“Tunatambua nguvu ya magrupu ya WhatsApp katika kufanikisha taarifa kwa jamii, hivyo Tanesco tumeona hili na hivyo kupitia Bodi yakatoka maagizo maalumu kwa wilaya zote na mikoa nchini kuhakikisha zinaanzisha magrupu hayo.

“Hivyo mameneja wa Tanesco kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa tayari wameanzisha magrupu hayo kwa ajili ya kuwasiliana na wateja”.

Muhaji alisema makundi hayo yatajumuisha wateja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Tanesco lengo ni kuhakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatolewa kwa wakati.

Alisema tangu kuanzishwa kwa makundi hayo tayari wameanza kuona matokeo chanya kwani hivi sasa wateja wao wanao uhakika wa kupata taarifa ya kila kinachoendelea na wakati huo huo wateja nao wanayo fursa ya kuwasilisha changamoto iwapo zitajitokeza.

Alisea  katika kuhakikisha makundi hayo yanaleta tija kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa walichokifanya ni kuweka makundi  kulingana na aina ya wateja.

Kwa sababu hiyo alisema  yapo makundi kwa ajili ya wateja wakubwa ambapo miongoni mwao wamo wawekezaji.

“Kuna makundi ya wateja wa kati na ya wateja wa kawaida kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.

“Tuliamua pia kwenye makundi hayo wawepo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali za Mitaa, Wakuu wa Wilaya, wabunge na viongozi wengine wa serikali ambao ni sehemu ya wadau muhimu katika kuhakikisha tunatatua changamoto za umeme.

“Kwa maana hiyo hata Mkurugenzi Mtendaji wa shirika letu katika mtaa anaoishi ameunganishwa kama mteja wa Tanesco kwenye grupu la WhatsApp na wakati huo huo kama kiongozi,” alisema

Leila ambaye yupo kwenye ziara ya wahariri wa vyombo vya habari mkoani Arusha yenye lengo la kuangalia miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano amesisitiza umuhimu wa makundi hayo ambapo wawekezaji wa mkoa huo wamekiri kuwa sasa imekuwa rahisi kwao kupata taarifa.

Wakizungumza na Mtanzania baadhi ya wamiliki wa viwanda waliopo mkoani Arusha , wamesema kwa sasa wanajiona wenye thamani kutokana na namna ambavyo Tanesco imeamua kuwaweka karibu kupitia njia hiyo ya kuwasiliana.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,464FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles