23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

TANESCO KUFUNGUKA LEO DENI LA SMZ

PATRICIA KIMELEMETA, Dar es Salaam


SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) leo linatarajia kuweka hadharani deni la Sh bilioni 121 inazowadaiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya Rais John Magufuli kuliagiza shirika hilo kuikatia umeme SMZ  baada ya kushindwa kulipa deni hilo   kwa ajili ya kusambaza umeme visiwani humo.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo wakati wa kuweka jiwe la msingi katika kituo cha kupooza umeme wa kilovoti 132 kilichopo Mtwara.

Alikuwa  kwenye ziara ya siku nne ya mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, wiki iliyopita.

  Ofisa Habari na Uhusiano wa Tanesco, Leyla Muhaji amesema  shirika  haliwezi kuficha suala hilo kwa sababu tayari Rais Magufuli amelizungumzia.

 Alisema  uongozi wa shirika hilo umepanga kutoa mchanganuo wa deni hilo tangu lilipoanza hadi lilipofikia wananchi waweze kulielewa.

“Hatuwezi kuficha deni la Zanzibar kwa sababu tayari Rais Magufuli ameliweka wazi.

“Mimi na viongozi wangu tutajipanga tuweze kutoa mchanganuo wa deni lenyewe tangu lilipoanza hadi lilipofikia, kwa sasa tupo safarini lakini kesho(leo), tutakuwa ofisini,”alisema Muhaji.

Alisema wataandaa taarifa hiyo ambayo itatolewa kwa waandishi wa habari waweze kuwahabarisha wananchi.

  Rais Magufuli alisema   suala la umeme lisigeuzwe kuwa la siasa.

Alisema wadaiwa sugu wa umeme wakatiwe umeme kwa vile  shirika hilo halipo kisiasa bali kwa utendaji, hivyo   wadaiwa sugu wote wanapaswa kulipa madeni hayo na   watakaoshindwa wakatiwe umeme hata kama ni Ikulu.

Alisema Tanesco inapaswa kufuatilia madeni yake popote kwa sababu wakati mwingine fedha zinakuwa zinatolewa wizarani lakini wanaona umeme siyo muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles