25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

ACHENI KULIA NJAA – MTAFITI

Na ASHA BANI- Dar es Salaam


SERIKALI imewashauri wananchi kuacha kulalamika njaa na badala yake kulima mazao ya mizizi na yanayostahimili ukame.

Hayo yalielezwa jana na  Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo ya Kilimo, Dk. Hussein Mansoor alipokuwa katika mkutano wa wataalamu wa mazao ya mizizi uliofanyika   Dar es Salaam jsns.

Alisema mazao ya mizizi yataleta mabadilko chanya endapo kutakuwa na ushirikiano wa nchi za Afrika nchi wanachama wenye nia ya dhati ya kutokomeza njaa katika maeneo mbalimbali ya Afrika.

Mkutano huo uliowakilishwa na wajumbe zaidi 300 una lengo la kuwakumbusha wananchi kulima mazao ya mizizi  kuondoa uhaba wa vyakula.

Alisema kwa Tanzania tayari aina ya mbegu 18 zimekwisha  kutangazwa na watafiti ziweze kutumika, ambazo aliamini zitaleta tija.

‘’Tusilie njaa kwa sababu ya kukosa mahindi  wakati vyakula vya muda vipo… mfano wa viazi vitamu na mihogo inavunwa kwa muda mfupi na wananchi wakanufaika nayo,’’alisema Dk. Mansoor.

Alisema Watanzania wanatakiwa kubadilika na kuongeza wigo wa vyakula wanavyokula hata majumbani.

Hata hivyo, alisema katika uzalishaji wa mazao hayo, kuna changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mbegu zake kwa kuwa  unatumia sehemu ya mmea.

Alisema kutokana na changamoto hizo tayari kampuni za watu binafsi zinahitajika katika kuzalisha mbegu hizo.

Kiongozi kutoka Taasisi ya Utafiti Kilimo kwa nchi za Tropic (IITA), Dk. Edward Karyu alisema    viazi vitamu na mihogo itasaidia katika ukame ingawa inahitajika mbolea nyingi.

Zaidi ya watafiti 300 ambao ni wabia wa maendeleo, watendaji wa sekta binafsi na wakulima  walihudhuria kongamnano hilo la 13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles