Tamasha la Sauti za Busara lazinduliwa

0
735

Jeremia Ernest, Zanzibar

MWENYEKITI wa bodi ya Busara, Muhamed Sumai ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu katika serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar, amezindua tamasha la Sauti za Busara msimu wa 17 katika eneo la kihistoria la Ngome Kongwe.

Tamasha hilo limekua likiwakutanisha wasanii kutoka nchi za Afrika kwa ajili ya kuonyesha vipaji vyao na kutoa burudania ya muziki.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo alisema ni furaha kuona wazo la watu saba leo limekuwa wazo la watu wengi ambao wanapata faida nalo.

“Tulianzisha tamasha hili watu saba leo hii limekua na mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, jamii inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na tamasha hilo,” alisema Muhamed Sumai.

Aliongeza kuwa miongoni mwa timu ya watu saba ni pamoja na marehemu Ruge Mutahaba ambae ametangulia mbele za haki. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here