Dudu Baya aachiwa huru

0
962

Beatrice Kaiza

MKALI wa bongo fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ kwa sasa ameachiwa huru baada ya kufungiwa kufanya kazi ya Sanaa kutokana na kukataa wito wa kuhojiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuhusu tuhuma za kutumia lugha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.

Kutokana na hali hiyo BASATA walimfungia msanii huyo kufanya kazi zake, lakini baada ya kuomba radhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michoze, Dk. Harrison Mwakyembe amemsamehe.

Akizungumza na MTANZANIA jana, msanii huyo alisema kwa sasa yupo huru baada ya kuupigia goti uongozi.

“Maombi yangu yamesikilizwa na Dk. Mwakyembe na kupewa msamaha na kila kitu kimekamilika, hivyo mashabiki zangu sasa wakae tayari kwa kazi mpya,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here