23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Tamasha la Octoberfest kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini

Upendo Mosha, Moshi

Killfair Promotion inakusudia kufanya tamasha kubwa la kimataifa lijulikanalo Kama Octoberfest lenye lengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini ikiwemo kinywaji cha bia.

Tamasha hilo ambalo linarajiwa kuhudhuriwa na wananchi zaidi ya 2000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki litalofanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia tamasha hilo kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Killfair Promotion, Dominic Shoo amesema tamasha hilo litakuwa na fursa ya bidhaa za Tanzania ikiwemo bia katika ngazi mbalimbali za kimataifa.

“Tamasha hili litafanyika Octoba  11 na 12 Mjini Moshi na lengo letu ni kutangaza bidhaa za hapa nchi ikiwemo vyakula na vinywaji vinavyozalishwa hapa nchi naamini baada ya tamasha hili bidhaa za hapa nyumbani zitapata soko” amesema Shoo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles