TANROADS, TARURA KUFANYA TATHIMINI YA UHARIBIFU ULIOSABABISHWA NA MVUA TANGA

0
596

Amina Omari, Korogwe

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigela amewaagiza Tanroads na Wakala ya Barabara Vijijini na mijini (TARURA) kufanya tathimini ya uharibifu wa miundombinu iliyotokana na athari za mvua mkoani humo.

Ameyasema hayo leo wakati alipowatembelea waathirika wa mafuriko katika wilaya ya Korogwe mkoani humo.

Amesema kuwa mvua hiyo imeweza kuleta athari kubwa za miundombinu pamoja na maeneo ya huduma za jamii.

“Niwaagize taasisi zinazohusika na miundombinu kufanya tathimini ili tujue athari zilizotokea na tuweze kupanga bajeti ya kushughulikia athari hizo” amesema RC Shigela.

Awali Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Timotheo Mzava amesema kuwa jumla ya nyumba 64 ziliweza kuzingirwa na maji kutokana namvua hizo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here