23.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

TALGWU yaeleza umuhimu wa wafanyakazi katika kukuza miji

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

CHAMA Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania ( TALGWU), kimesema mafanikio yanayopatikana katika ukuaji wa miji unachangiwa na utendaji kazi bora katika sekta mbalimbali, hivyo haki za wafanyakazi ni muhimu katika undelezaji wa miji.

Akizungumza na waandihi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha Siku ya Miji Duniani inayofanyika kila mwaka Oktoba 31, Katibu Mkuu wa TALGWU, Rashid Mtima amesema haki za wafanyakazi ni sehemu muhimu ya ukuaji endelevu wa miji hapa nchini na duniani kote.

“TALGWU inatambua kazi inayofanyika katika miji hapa nchini hasa usimamizi wa miundombinu ya barabara, usafi wa mazingira, utunzaji wa taka ngumu na maji pamoja na shughuli zote za maendeleo zinazolenga kukuza miji hapa nchini, zinazofanywa na watumishi wa umma ambao ni wanachama wetu,” amesema Mtima.

Amesema mafanikio yanayopatikana katika ukuaji wa miji unachagizwa na utendaji bora, jukumu lao ni kuhakikisha eneo la kazi linakuwa salama bila manung’uniko na kutoa kipaombele kuhusu haki ya watendaji hao.

Amesema TALGWU inatambua jukumu hilo na wanahitaji wafanyakazi wawe katika mazingira bora na salama huku wakipatiwa hazi za msingi ambazo zitawaongezea ari na morali ya kufanya kazi kwa ubora.

Mtima amesema kuwa siku ya Miji duniani hutumika kama fursa ya kukuza nia ya Jumuiya ya Kimataifa, kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi katika kushughulikia changamoto za ukuaji wa miji na kuchangia maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles