31.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania, Ujerumani kuimarisha ushirikiano

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema lengo la ziara ya Rais wa Ujerumani, Dk. Frank-Walter Steinmeier ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliodumu kwa zaidi ya miaka 60.

Akizungumza leo Oktoba 31,2023 na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania ipo tayari kwa mazungumzo yajayo ya ushirikiano ambayo yatafanyika mwakani.

“Katika hili tumezielekeza timu za wataalamu wa Tanzania na Ujerumani kuendelea na mazungumzo ya mara kwa mara kuboresha maeneo ya ushirikiano, nimemkahikikishia Mh.Rais kwamba Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa mazungumzo yajayo ya ushirikiano yatakayofanyika mwakani,” amesema Rais Samia.

Amesema uhusiano huo wa kirafiki umepiga hatua nyingine ambapo ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani unahusisha pia sekta ya maji, afya, matumizi endelevu ya rasilimali na ulinzi wa mazingira, utawala bora wa fedha, usawa wa kijinsia na michezo.

“Suala la bima ya afya tulitaka usaidizi kwao watusaidie, serikali ya Ujerumani inajenga hospitali kubwa ya Jeshi Dodoma pia tuliomba watusaidie kujenga hospitali kubwa ya kisasa ya maradhi ya kuambukiza Lugalo,”amesema.

Aidha amesema katika utawala mambo mengi yamepita, hivyo watafungua majadiliano na kuona jinsi watakavyoweza kukubaliana kwa yale yaliyopita wakati wa utawala wa Ujerumani hapa nchini.

“Kufungua majadiliano ya kihistoria ni vipi watafanya, najua kuna familia ambazo zinasubiri mabaki ya ndugu zao yapo katika makumbusho mbalimbali Ujerumani hivyo tunafanya mazungumzo kwenda nayo vizuri,” amesema.

Kwa upande wake Dk. Frank-Walter Steinmeier amesema kupitia ziara yake Tanzania amejifunza mambo mengi na kubaini kuwa kuna makampuni mengi machanga ya uwekezaji na anatarajia kukutana na wabunifu hao vijana.

Amesema anatarajia kukutana na vijana wajasiriamali wa Kitanzania wanaojihusisha na uvumbuzi wa teknolojia mpya hasa matumizi ya akili bandia na kuahidi kuwa Ujerumani itawasimamia na kuwapatia mitaji.

“Nimefurahishwa na hili ningependa kusema kuwa tutawasimia hawa vijana wabunifu katika suala la ushiriki wa tukiangalia namna ya kutoa mitaji kwa kuwasaidia kwenye kuongeza uzoefu na maarifa kwenye sekta ya uchumi wa kidigitali,”amesema.

Dk. Stermier amesema kupitia kongamano la Jumuiya ya wafanyabishara kati ya Tanzania na Ujerumani kutasaidia kufanya kazi kwa ukaribu na kukuza uchumi na uhusiano kati nchi hizo mbili kuwa na nguvu zaidi hadi kwenye siasa na maeneo mengi.

Aidha amesema anatarajia kwenda mkoani Ruvuma kuonana na waathirika wa vita vya maji maji na kuzungumza nao na kuangalia kurudisha mabaki yaliyopo Ujerumani, “amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles