25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana wachangia uzalishaji ajira 89,509

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema vijana wamechangia kuzalisha ajira zaidi ya 89,509 na kuvutia uwekezaji wa zaidi ya Dola za Kimarekani 328 milioni katika miaka mitatu iliyopita.

Nape ameyasema hayo wakati wa kufungua kikao cha wadau wa TEHAMA katika kujadili mashirikiano ya mpango wa uandaaji wa sera ya kusimamia ubunifu na kampuni changa nchini, Oktoba 30,2023 jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa juhudi hizo ni pamoja na utoaji wa mazingira wezeshi ya sera na udhibiti, ambapo wizara hiyo kupitia TEHAMA imeanzisha mfumo wa udhibiti wa ‘Sandbox’ ili kusaidia ukuaji wa waanzilishi wa biashara ndogo na za kati ambao utaharakisha uanshiaji na utekelezaji.

“Katika enzi hizi za kidijitali, vijana nchini Tanzania wako mstari wa mbele kuunda bidhaa na huduma za kibunifu zinazoshughulikia masuala muhimu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira, ni muhimu kutambua kwamba sekta ina jukumu muhimu katika ajira na kuunda kazi,” amesema Nape.

Amesema serikali kupitia wizara hiyo inatambua nguvu ya mabadiliko ya waanzishaji wa kampuni katika kukuza uchumi.

“Mkutano huu unaonyesha dhamira ya dhati inayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira ya ubunifu, kuhimiza ukuaji wa sekta na maendeleo ya vipaji vinavyohusiana na teknolojia,” amesema.

Aidha amependekeza kila mdau katika kikao hicho, kuwasilisha jinsi atakavyoweza kuchangia uundaji wa sera kwa kuwa wizara ipo tayari kuwasiliana nao zaidi kwa msaada wowote ikiwa pamoja na mawazo ya kujenga utaalamu na njia njema katika utungwaji wa sera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles