24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

JKT Queens kuingia kifua mbele Ligi Mabingwa Afrika

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TIMU ya JKT Queens inatarajia kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Novemba 5,2023, huku uongozi wa timu hiyo ukiweka bayana kuwa wanajiamini.

Mchezo wa pili wa makundi ambapo JKT Queens ipo kundi A, itamenyana na wenyeji Athletico Abidjan Novemba 8, kisha kumaliza na SC Casablanca ya Morocco Novemba 11, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31, 2023, JKT Mlalakuwa, jijini Dar es Salaaam, Ofisa Habari wa JKT Queens, Masau Bwire amesema wanaingia katika michuano hiyo kifua mbele kwa kujiamini kutokana na ubora wa kikosi chao .

Ofisa Habari wa JKT Queens ,Masau Bwire

Amewatoa hofu watanzania kuwa wapinzani wanaokutana nao katika kundi A, wamewafuatilia na wanawafahamu vizuri, hivyo wataingia uwanjani wakijua wana jukumu kubwa la kuipambania Tanzania.

“Wapo baadhi wamekuwa wakisema tupo katika kundi gumu na wana mashaka nini tutakwenda kufanya huko.Niwatoe hofu watanzania, niwaaminishe kwamba timu yetu ni bora, tunao wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa, wameandaliwa na wako tayari.

Ameeleza lengo lao ni kwenda kucheza na kushinda na kupigania kombe lililoandaliwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kufikia tamati Novemba 19,2023.

“Lengo na dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba kupata sapoti kwa watanzania kwa sababu JKT Queens inaliwakilisha Taifa, inabeba bendera ya Taifa kwenda katika mashindano haya, lakini pia ukanda huu wa CECAFA,” amesema Bwire.

Amesema kikosi chao kinatarajia kuondoka kesho alfajiri kuelekea Ivori Coast kikiwa na wachezaji 21 na viongozi saba.

JKT Tanzania imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa CECAFA kwa kuifunga CBE ya Ethiopia kwa mikwaju 5-4 ya penalti katika mchezo wa fainali uliopigwa Agosti 30, 2023 nchini Uganda.

Msimu uliopita katika michuano hiyo, Tanzania iliwakilishwa na Simba Queens ambayo ilifanikiwa kufika nusu fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles