22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

TAKUKURU yamdaka Mhasibu TPA akiwa mafichoni Mwanza

Na Sheila Katikula, Mwanza

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza imemkamata aliyekuwa Mhasibu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Mkoa wa Kigoma, Madaraka Madaraka ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya Rushwa, uhujumu uchumi na ukwepaji wa zaidi ya Sh milioni 153.

Hayo aliyasema jana na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Frank  Mkilanya wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake  mkoani hapa.

Amesema mtuhumiwa  huyo amekamatwa akiwa mafichoni  katika eneo la nyasa Wilayani Ilemela ambapo alikuwa akitafutwa   na Takukuru tangu Mwezi Agosti 2020 ili aweze kuunganishwa kwenye tuhuma hiyo na wenzake watano ambao walifikishwa  Katika mahakama ya hakimu mkazi  Mkoani Kigoma Agosti 31, mwaka jana.

“Washtakiwa hao ni Rodrick Ndeonasia ambaye alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Saxon Building Contractors Limited, Ajuaye Msese aliyekuwa Meneja wa bandari Kigoma, Herman  Shimbe aliyekuwa afisa uhasibu TPA  Kigoma, Jesse Mpenzile aliyekuwa Mhandisi mkazi TPA Kigoma, Lusubilo Mwakyusa aliyekuwa afisa rasimali watu TPA Kigoma,” alisema.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha Januari hadi Machi Mwaka huu Takukuru Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kuokoa fedha zaidi ya Sh milioni 87 ambazo zililejeshwa kwenye msako wa kufatilia fedha za umma zilizokuwa zimechepushwa na kufanyiwa anyiwa ubadhilifu kinyume na Sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na vile vile imefungua kesi mpya nane.

Alisema kati ya fedha hizo zilizookolewa kiasi Cha Sh milioni 14 zimewekwa kwenye akaunti maalumu iliyopo Benki Kuu na sh milioni 73 zimerejeshwa kwa wahusika baada ya kuokolewa.

Aidha, Mkilanya akisema Sh 38,006,275 zimerejeshwa kwa wakurugenzi wa halmashauri, Sh milioni 4,345,000 zimekabidhiwa kwa vyama vya ushirika Sh 18,539,200 zimerejeshwa kwa wananchi waliodhulumiwa kupitia mikopo umiza na Sh 12,267,800 zimekabidhiwa kwa watumishi wa sekta binafsi ambao walifanyakazi bila kupata stahiki zao kutoka kwa waajiri.

Alisema Katika kipindi hicho Takukuru mkoani hapa imekamilisha uchunguzi wa majalada 12, imefungua kesi mpya nane na kupokea taarifa 280 za malalamiko ya vitendo vya Rushwa.

Alisema katika kipindi hicho  piavTakukuru mkoani hapa imeweza kuzuia  vitendo vya rushwa kwa kutoa elimu na kuyafikia makundi mbalimbali kwa kufanya semina 37 mikutano ya hadhara 57, vipindi vitano vya radio, Waandishi wa Habari, makala tisa, na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari vinne maonesho 13 na kuimarisha klabu 83 za wapinga rushwa kwenye shule za msingi, Sekondari na vyuo.

“Tunaendelea na  kutekeleza utaratibu  wa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao  ili kutatua kero zinazotokana na vitendo vya rushwa utaratibu huu unaitwa Takukuru inayotembea  na tumebaini hadi hivi sasa idara za Serikali zinatakiwa kuelimisha wananchi juu ya huduma wanaziozitoa ili kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi,” alisema Mkilanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles