23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Pata habari kubwa za michezo hapa

London, Uingereza

Mourinho kuinoa Celtic
Imebainika kuwa Jose Mourinho anaweza kutangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Celtic ya Ligi Kuu ya Scotland.
Wakati huo huo, Mourinho aliyefungashiwa virago Tottenham juzi anawindwa na Valencia ya Ligi Kuu ya Hispania.
CHANZO: Sun

Aguero apewa miwili Barca
Barcelona wamempa ofa ya mkataba wa miaka miwili straika wa Manchester City na timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero.

Aguero (32), ataondoka Man City mwishoni mwa msimu huu, ambapo atakuwa ameshamaliza mkataba wake na klabu hiyo.
CHANZO: TyC Sports

Liver waikamua Porto bil. 27/-

MABOSI wa Liverpool wanataka Pauni milioni 8.63 ili wairuhusu Porto kubaki na kiungo Marko Grujic.
Grujic raia wa Serbia, kwa sasa anaitumikia kwa mkopo klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ureno.
CHANZO: A Bole

Alaba miaka mitano Madrid

Imefichuka kuwa beki wa Bayern Munich, David Alaba, amekubali ofa ya mkataba wa miaka mitano iliyowasilishwa na Real Madrid.

Hii ni habari mbaya kwa klabu za Chelsea na Manchester City, ambazo kila moja imekuwa ikimtolea macho raia huyo wa Austria. CHANZO: Sky Sport Germany

Anayetakiwa United azuiwa

West Bromwich Albion inataka kumbakiza kwa gharama yoyote mlinda mlango wake raia wa England, Sam Johnstone.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28, anawavutia mabosi wa klabu za Manchester United, pia akiwaniwa na West Ham.
CHANZO: Express and Star

Arsenal kumzuia kipa

Washika Bunduki wa London, Arsenal, wako kwenye hatua nzuri ya kumsajili moja kwa moja mlinda mlango Mat Ryan.
Kwa mujibu wa taarifa, mazungumzo kati ya Arsenal na klabu yake, Brighton & Hove Albion, yanaendelea vizuri.
CHANZO: Football Insider

Mbappe asaka nyumba Madrid
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe, ameripotiwa kuanza kutafuta mjengo jijini Madrid, Hispania.
Taarifa hiyo inaibua upya tetesi za Mfaransa huyo kutakiwa na vigogo wa La Liga, Real Madrid.
CHANZO: Goal

Vigogo England wajitoa ESL

LABU za Manchester United, Liverpool, Arsenal na Tottenham Hotspur zimejitoa kwenye michuano mipya ya European Super League (ESL).

Timu hizo zilikuwa kati ya zile 12 zinazotajwa kuanzisha ESL, mashindano yanayopigwa vita kwa kuwa inalenga kuua ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man City imekuwa timu ya kwanza kuipa kisogo michuano hiyo inayotajwa kuwa tajiri wa zaidi ya mara mbili wa ule wa Ligi ya Mabingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles