30.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Takukuru kuwahoji tena kina Malinzi

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeridhia ombi la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), la kuwachukua aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa kwa ajili ya kuwahoji.

Takukuru ikiwakilishwa na Wakili Leonard Swai, ametoa maombi hayo leo Jumatano Januari 16, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri. “Mheshimiwa upande wa Jamhuri tunaomba kuwachukua mshtakiwa wa kwanza na wa pili kwa ajili ya mahojiano, kuna kitu tunataka kuongezea,” alidai Swai.

Hakimu Mashauri alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hadi Januari 21 ambapo shahidi wa tisa wa Jamhuri atatoa ushahidi. Washtakiwa katika kesi hiyo mbali na aliyekuwa rais TFF, Jamal Malinzi (57) wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine (46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27).

Wengine ni Meneja wa Ofisi ya TFF, Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335 na Sh 43,100,000.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles