23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yawasilisha majukumu yake kwa kamati ya Afya na masuala ya UKIMWI

Na Nadhifa Omar, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano unaostahiki kwa kamati ya Afya na masuala ya UKIMWI kutekeleza majukumu kwa kufuata miongozo,maoni na ushauri mnaoutolewa na kamati hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo akizungumza na wajumbe pamoja na watendaji wa TACAIDS na Ofisi ya Waziri Mkuu waliohdhuria kikao cha kamati hiyo walipokutana leo jijini Dodoma.

Kauli hiyo amaitoa leo Machi 12, 2023 baada ya Tume ya kudhibiti UKMWI Tanzania (TACAIDS) kuwasilisha taarifa kuhusu muundo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Awali, akiwasilisha taarifa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amesema TACAIDS ni Idara inayojitegemea chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na imeanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.22 ya mwaka 2001 na Marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015, sheria hiyo ni kwaajili ya Tanzania bara pekee, Zanzibar ipo Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

Dk. Maboko ameyataja majukumu ya TACAIDS kuwa ni kuandaa sera na miongozo kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini pamoja na kusimamia athari zake, kisimamia mpango mkakati kwa ajili ya mipango ya programu za UKIMWI pamoja na masuala mtambuka yahusuyo virus vya UKIMWI na UKIMWI.

Kujenga mahusiano ya kitaifa na kimataifa kwa watu wote wa UKIMWI kwa kufanya uratibu wa masuala ya UKIMWI, kutafuta raslimali fedha, kuzigawa na kuzifuattilia katika programu za Mwitikio wa UKIMWI,kusambaza taarifa kuhusu UKIMWI na madhara yake na kwa programu kwa kuzuia na kudhibiti.

Kukuza tafiti, upashanaji taarifa na kutunza kumbukumbu zinazohusiana na udhibiti wa UKIMWI nchini, kukuza uraghibishi na utoaji wa elimu kwa angazi ya juu kuhusu kuhusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI, kufuatilia na kutathimini shughuli zote za UKIMWI zinazotekelezwa nchini.

Dk. Leonard Maboko, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS akiwasilisha Muundo, na Majukumu ya TACAIDS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakati wa kikao kilichfanyika leo jijini Dodoma Machi 12, 2023.

Aidha, ameongeza kuwa shughuli nyingine ni Kuratibu shughuli zote za UKIMWI na kuzisimamia kwa mujibu wa mkakati wa Taifa wa UKIMWI, kwa kushirikiana na sekta binafsi husika kuwezesha juhudi za upatikanaji wa tiba na kuhamasisha upatikanaji wa tiba na matunzo na chanjo.

Jukumu lingine ni kuhamasisha haki na wajibu kwa watu wanaoishi na VVU kuhamasisha WAVIU kuishi kwa matumaini na kushauri serikali kuhusu masuala yote yanayohusu kuzuia na kudhibiti  UKIMWI, kutambua vikwazo katika utekelezaji wa kuzuia na kudhibiti katika sera na programu, kusimamia shughuli zote zinazohusiana na kuzuia na kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI na kushirikiana na sekta nyingine husika, kufanya shughuli nyingine za kuzuia na kudhibiti VVU na UKIMWI.

Dk. Maboko amesema utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS unaongozwa na sera, sheria, kanuni, mikakati na miongozo ikiwa ni pamoja na sheria ya tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania Na. 22 ya mwaka 2001 na marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015, Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001.

Seif Salum Seif mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo na TACAIDS kuhusu kubadilisha jumbe zinazotumika kwenye vibao vya ujenzi vinavyotumia maneno ya Unayanyapaa.

Mwongozo wa uraghibishi na mabadiliko ya tabia,Mwongozo wa VVu na UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoabikiza, mwongozo wa kusshughulikia makundi maalum kuhusu UKIMWI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, mwongozo wa jinsia na UKIMWI, mwongozo wa UKIMWI na haki za binadamu, mwongozo wa kufundishia kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za Halmashauri,kata na vijiji, pamoja na mwongozo wa kuunda kamati za kudhibiti UKIMWI kwenye mikoa, mwongozo wa kuunda Kamati za kudhibti UKIMWI kwenye Halmashauri.

George Simbachawene Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Katibu Mkuu, Dk. Yonaz Jimmy wakimsikiliza, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko alipokuwa anawasilisha Muundo na Majukumu kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, leo Machi 12, 2023 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo ameipongeza TACAIDS kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kudhibiti na kupunguza maambukizi ya VVU nchini na kiagiza kuendelea kufanyia kazi ushauri na maekezo yaliyotolewa na kamati hiyo,ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji wa utekelezaji wa majukumu wa kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles