25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

Tacaids: Unyanyapaa bado ni kikwazo

Na Faraja Masinde


TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya  Ukimwi umezidi kuwa kikwazo katika kukabiliana na maambukizi mapya  ya ugonjwa huo.

Pamoja na changamoto hiyo unyanyapaa umechangia kwa kiwango kikubwa wenye maambukizi kutokuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi na kujenga hofu kwa watu kwenda kupima na kupata unasihi kwa wataalamu.

Mpaka sasa kwa mujibu wa Tacaids kundi kubwa la vijana kuanzia miaka 15-24 ndilo limekuwa katika hatari ya kupata maambukizi mapya ambapo kitaifa hali ya maambukizi mapya kwa vijana ni asilimia 40. Katika kundi hilo, vijana wa kike ni asilimia 80 huku wakiume ikiwa ni asilimia 20.


Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Afisa wa Vijana wa Tacaids, Dk. Kafura Wiliam wakati akizungumza katika Semina maalumu ya kuwajengea uwezo Majaji wa Shindano la kuibua vipaji kwa Vijana ‘Bongostar Search’ kwa lengo la kuzungumza lugha rafiki kwa Vijana juu ya ugonjwa wa ukimwi. Alisema jamii inapaswa kuepukana na lugha za kukatisha tamaa hasa kwa waliogundulika kuwa na maambukizi ya ukimwi kwani lugha hizo ni hatari kuliko ugonjwa wenyewe.

Alisema takribani asilimia 80 ya maambukizi ya ukimwi watu walidhani yanatokana na mume na mke jambo ambalo lilitengeneza hisia hasi katika jamii kwamba Ukimwi unatokana na zinaa.

Dk.Kafura alisema ukimwi upo katika makundi maalumu hasa wanaofanya biashara ya ngono, wanaojidunga dawa za kulevya  na wengineo hali aliyosema kuwa kiwango chao cha maambukizi ni kikubwa, nakwamba  hawapaswi kunyanyapaliwa ili kufikia lengo la kutokomeza maambukizi mapya ya Ukimwi.

“Ukipima kiwango cha maambukizi katika makundi haya ni mara nne mpaka 10 ya watu wote, ukimchukua mtu anayefanya biashara ya ngono, anayejidunga dawa za kulevya ukiwapima kiasi cha maambukizi ni kubwa, mfano dada wanaofanya biashara ya ngono kasi ya maambukizi ya ukimwi kwao ni asilimia 36.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles