23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

T.I na Tiny wanatarajia mtoto wa pili

Celebrities at The AXE Lounge in SouthamptonNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa hip hop nchini Marekani T.I na mke wake, Tiny wanatarajia kupata mtoto wao wa pili hivi karibuni

Endapo watafanikiwa kupata mtoto huyo basi T.I atakuwa na jumla ya watoto sita, lakini kwa Tiny atakuwa na watoto watatu.

“Ni furaha kubwa kuona familia yetu inaongezeka, tunatarajia kupata mtoto hivi karibuni, hii ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alisema Tiny.

T.I ni miongoni mwa wasanii ambao wana watoto wengi nchini Marekani kama vile DMX ambaye ana watoto 12.

Kupitia mtandao wa Instagram, Tiny aliweka picha yake na kudai kwamba wanashukuru Mungu kwa kuwapa zawadi mpya.

“Tuna furaha kubwa sana kwa zawadi ambayo tunaitarajia hivi karibuni ya mtoto ambaye yuko njiani kwa sasa,” aliandika Tiny.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles