24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Syria yaonywa matumizi ya kemikali

NEW YORK, Marekani

MSHAURI wa  Usalama wa Taifa nchini hapa, John Bolton ameionya Serikali ya Syria akisema isidhani kuwa hatua inayosubiriwa ya kuondosha majeshi kutoka nchini humo kama ni ruhsa ya wao sasa kutumia silaha za kemikali.

Mshauri huyo aliyasema hayo juzi na kwamba msimamo wa serikali ya nchi hii hauna mabadiliko dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali ambazo zinatumiwa na serikali ya Syria.

“Hakuna kabisa mabadiliko juu ya msimamo wa Marekani dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali zinazo tumiwa na utawala wa Syria.

“Hakuna mabadiliko kwamba matumizi yoyote ya silaha za kemikali yatakabiliwa na hatua kali sana, kama tulivyokuwa tumefanya mara mbili hapo awali,” Bolton aliwaambia waandishi akiwa katika ndege yake muda mfupi kabla ya kutua mjini Tel Aviv nchini  Israel.

“Kwa hiyo utawala wa Assad usijidanganye juu ya suala hilo, wakati tukifafanua jinsi utaratibu wa kuondoa majeshi utakavyo kuwa na mazingira yake, hatutaki utawala wa Assad kuangalia hatua hii kuwa inapunguza shinikizo letu dhidi ya matumizi ya silaha za maangamizi ya umma,”aliongeza Bolton.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles