29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya Uchaguzi DRC yaahirisha kutoa matokeo

KINSHASA, Congo DRC

TUME ya  Uchaguzi nchini hapa imechelewesha kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais, huku kukiwa na ongezeko la shinikizo kutoka mataifa yenye nguvu na Kanisa Katoliki kuheshimu matakwa ya wapiga kura.

Mkuu wa tume hiyo, CENI aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP,  kwamba matokeo ya  awali, ambayo  yalipangwa kutolewa jana  sasa yatatolewa  wiki  ijayo masaa  machache kabla  ya  muda  wa  mwisho  kumalizika.

“Haitawezekana  kutangaza  matokeo  siku  ya leo (jana). Tunapinga hatua, lakini  hatuna  kila  kitu bado,” alisema Corneille Nangaa bila ya  kueleza siku ya kutangaza  matokeo hayo.

Baraza  la maaskofu  wa  Kanisa  Katoliki  lenye ushawishi  mkubwa nchini  hapa , CENCO, ambalo  linawakilisha  maaskofu  wa kikatoliki  nchini  kote , limeonya  kwamba  hasira za umma zinaweza  kujitokeza iwapo matokeo  ya  mwisho hayatakuwa  ya kweli kwa mujibu wa matokeo halisi  ya kura.

Kanisa katoliki  lenye ushawishi nchini, ambalo limetoa  zaidi ya  wachunguzi  40,000 , lilisema   mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba  linamjua mshindi  wa  uchaguzi  huo, lakini  halikumtaja.

Katika  barua iliyotumwa kwa Nangaa  juzi,  Rais  wa  Baraza la  CENCO,  Marcel Utembi alisema kutokana  na ucheleweshaji huo, iwapo  kutakuwa  na  vuguvugu  la  maandamano ya  umma  litakuwa  ni  jukumu  la  CENI.

Uchaguzi  huo  wa  Desemba 30 ulishuhudia wagombea  21 wakipambana  kuwania  kuchukua  nafasi  ya  Rais Joseph  Kabila, ambaye  ameitawala  nchi  hii  kubwa , iliyokumbwa  na  mizozo kwa karibu miaka  18.

Miongoni  mwa wale  walioko  katika  nafasi  za  mbele ni  pamoja  na mrithi  aliyeteuliwa  na Rais  Kabila Emmanuel Ramazani Shadary  na wagombea  wawili  wa  upinzani, mwanasiasa wa siku  nyingi mwenye  ushawishi  mkubwa Felix Tshisekedi  na Martin Fayulu ambaye  amejitokeza  hivi  karibuni.

Anayetafutwa  ni mwanasiasa kiongozi  katika  nchi  hiyo  yenye utajiri  mkubwa  wa  madini  ambayo  haijawahi  kuwa na kipindi  cha madadiliko  ya  amani  ya  utawala  tangu  ipate   uhuru kutoka  Ubelgiji  mwaka  1960.

Kabila alikuwa  aondoke  madarakani  miaka  miwili  iliyopita, lakini aling’ang’ania  madarakani na  kuzusha  maandamano  ya  umma ambayo  yalikandamizwa kikatili, na  kusababisha vifo vya   watu  kadhaa.

Uchaguzi ambao  ulitanguliwa  na  kucheleweshwa  mara  kwa mara, ulifanyika   katika  hali  ya  utulivu, lakini  hali  ya  wasi wasi imejijenga  katika  muda  wa  kipindi  cha  mchakato  wa  kuhesabu kura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles