26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

SUGU AANZA BUNGE KWA KUPARURANA NA CHENGE

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), maarufu Sugu, ameingia bungeni kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani kwa msamaha na rais, huku akiparurana na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyekuwa akiongoza kikao cha jana mara baada ya kupewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mbali na hilo, Sugu pia alisababisha kipindi cha maswali na majibu kisimame kwa dakika moja kutokana na wabunge kumshangilia mara alipoingia bungeni.

Sugu alitoka gerezani Mei 10, mwaka huu kutokana na msamaha wa Rais Dk. John Magufuli kwa wafungwa, alioutoa wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano, Aprili 26.

 

AKIULIZA SWALI

Mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, kujibu swali la msingi la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) lilohusu sheria za makosa ya mtandao, Mwenyekiti wa Bunge, Chenge, alimruhusu Sugu aulize swali la nyongeza.

Akiuliza swali lake, Sugu aliwataka viongozi kuutumia mwezi wa Ramadhan kujitafakari.

“Asante Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatakie mfungo mwema ndugu zangu Waislamu, ndani ya Bunge na nchi nzima, kwa wale ambao ni viongozi, wautumie mwezi huu kujitathmini,” alisema.

Kutokana na kauli hiyo, Chenge alimweleza Sugu aulize swali moja kwa moja.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles