23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Sudan yataka kuondolewa orodha ya ugaidi

KHARTOUM, SUDAN

SERIKALI ya Sudan imetoa taarifa ikiiambia Marekani kwamba suala la kuondolewa jina la Sudan katika orodha ya magaidi halipasi kushurutishwa na kuanzisha uhusiano wa kidoplomasia na utawala haramu wa Israel.

Msemaji wa Serikali ya Sudan,  Faisal Mohamed Saleh alisema katika taarifa hiyo kwamba, katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo aliyetembelea Khartoum, Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok aliitaka Washington isifungamanishe suala la kuondolewa jina la Sudan katika orodha ya magaidi na kadhia ya kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.

Hii ni baada ya duru za habari kutangaza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo anafanya safari katika nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu katika mikakati ya kuzishawishi nchi hizo zianzishe uhusiano na utawala haramu wa Israel.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok juzi Jumanne alimwambia Pompeo kwamba Khartoum haiwezi kuanzisha uhusiano na Israel katika kipindi hiki. 

Nchi nyingi za Kiislamu zimepinga suala la kuanzisha uhusiano na utawala  wa Israel

Hamdok alimweleza Pompeo kwamba serikali ya mpito ya Sudan ambayo ilishika hatamu baada ya kuondolewa madarakani Omar al-Bashir mwaka jana haina mamlaka ya kuchukua hatua kama hiyo. 

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,642FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles