24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyepigwa risasi ‘atahitaji miujiza’ kutembea

WISCONSIN, MAREKANI

MAWAKILI wa familia ya mtu mweusi aliyepigwa risasi na polisi katika Jimbo la Wisconsin nchini Marekani wanasema anahitaji “miujiza” kutembea tena.

Jacob Blake, 29, alipigwa risasi mara kadhaa akifungua mlango wa gari mjini Kenosha. Moja ya risasi alizopigwa ilipitia katika uti wake wa mgongo, mawakili wanasema.

Kupigwa risasi kwa Blake kumetibua maandamano na ghasia wakati mwingine. Gavana wa Wisconsin ametuma wanajeshi zaidi wa ulinzi wa kitaifa Kenosha.

Blake kwa sasa amepooza, na madaktari hawana hakika ikiwa atafanikiwa tena kutumia miguu yake. 

“Familia yake inaamini miujiza inaweza kutokea, lakini matokeo ya uchunguzi wa kimatibabu yanaonesha kwa sasa amepooza, kwa sababu risasi hizo zilijeruhi uti wake wa mgongo, itakuwa miujiza kwa Jacob Blake Jr kutembea tena,” wakili Ben Crump aliwaambia wanahabari siku ya Jumanne.

Mtu huyo aliye na miaka 29, alipigwa risasi mbele ya wanawe wa kiume waliokua ndani ya gari, aliachwa na mashimo ya risasi tumboni, kujeruhiwa mkono pamoja na figo na ini lake. Sehemu kubwa ya utumbo wake ulitolewa, mawakili wake waliwambia wanahabari.

Mama yake, Julia Jackson aliwafahamisha wanahabari kwamba mwanawe “anapigania maisha yake”, lakini angelijua kinachoendelea kwa sasa, maandamano na uharibifu, hangelifurahia hata kidogo”.

Picha kutoka mji huo uliopo kilo mita 100,000 kusini magharibi mwa ufuo wa Ziwa Michigan zinaonesha majengo na magari yalioharibiwa kufuatia maandamano ya siku mbili nyakati za usiku kupinga ukatili wa polisi.

Siku ya Jumanne, Gavana Tony Evers alisema atawapeleka walinzi zaidi wa kitaifa mjini Kenosha kuchunguza majengo ya serikali na kuwapa ulinzi wazima moto. Hali ya hatari pia imetangazwa Wisconsin.

Tukio la kupigwa risasi kwa Blake limetokea wakati ambapo idara ya polisi nchini Marekani inakabiliwa na tuhuma za kuwanyanyasa Wamarekani weusi, huku suala la ubaguzi wa rangi likiendelea kuwa chanzo cha mgogoro katika jamii, tangu kifo cha Mmarekani mwingine mweusi mikononi mwa polisi mjini Minneapolis, George Floyd, mwezi Mei.

Katika taarifa yake, Jackson aliangazia moja kwa moja suala la ubaguzi wa rangi na kutoa wito wa “mshikamano”.

Polisi walisema kuwa walikuwa wakishughulikia mzozo wa kifamilia kabla ya kufika katika eneo la tukio siku ya Jumapili lakini hawakutoa maelezo zaidi. Kufikia sasa haijabainika ni nani aliyewapigia simu polisi, ni wangapi walihusika na tukio hilo, na nini kilichokea kabla ya Blake kupigwa risasi.

Kanda ya video ya tukio hilo inamuonesha Blake akifungua mlango na kisha kuegemea upande wa ndani hali ambayo ilimfanya polisi kumshika mashati na kuanza kumpiga risasi. 

Milio saba ya risasi inasikika katika video hiyo, huku walioshuhudia wakipiga mayowe.

Mchumba wa  Blake, Laquisha Booker, alisema watoto walioshuhudia kila kitu kilichotokea walikaa nyuma ya gari wakipiga mayowe wakati baba yao anapigwa risasi.

Mawakili Blake walisema alikuwa akijaribu “kuzuia kutokea kwa mzozo wa kinyumbani”. Mashuhuda pia waliwaambia wanahabari mjini humo.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles