28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Sudan yaadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi dhidi ya Bashir ikiwa hoi

KHARTOUM, SUDAN

SUDAN imetimiza mwaka mmoja tangu kuondolewa kwa Rais Omar al-Bashir. Lakini hakuna cha  kusherehekea. 

Uchumi bado uko dhaifu, hali ya kisiasa bado ni tete, huku janga  la virusi vya corona likizusha mtafaruku mwingine.

Mwaka mmoja  uliopita , mamia  kwa  maelfu ya  raia  wa  Sudan  walifanya maandamano  ya wiki  nzima mbele ya  makao makuu  ya  jeshi  katika  mji mkuu  wa  nchi  hiyo  Khartoum.

Mwanafunzi kijana  mwanamke, Alla Salah, alisimama  juu  ya  gari  akiimba kauli mbiu za kisiasa, baadaye  alikuja  kuwa  ishara  ya  vuguvugu la maandamano  katika jamii  ambayo  kwa  kiasi  kikubwa  inadhibitiwa  na  wanaume zaidi.

Kila  mmoja  aliingia  mitaani, ikiwa  ni  pamoja  na  maprofesa, waalimu  na  madaktari. 

Wasanii waliandika  ujumbe  na kuchora   picha za  uhuru katika  kuta mjini  Khartoum.

Kwa miezi  kadhaa , nchi  hiyo  ilikuwa  ikitokota  hadi  hatimaye  kile  ambacho hakikufikirika  kikatokea.

Rais Omar al-Bashir alipinduliwa  Aprili 11, 2019, baada  ya kukaa madarakani karibu miaka 30.

Yalikuwa  mapinduzi  yaliyoelezwa  na  wengi  kuwa  ni vuguvugu  la  mapinduzi ya  mataifa ya  Kiarabu namba  mbili. 

Lakini  mwaka  mmoja  baadaye, katika  kusherehekea  mwaka  mmoja  wa siku hii  kubwa, hali mjini  Khartoum imenyong’onyea.

Kwasababu  ya  janga  la  virusi  vya  corona, shule  na  vyuo  vikuu vimefungwa. Sherehe  za maadhimisho , kupeperusha  bendera na kuimba wimbo  wa  taifa  ama  nyimbo  za mapinduzi, vimefanyika  nyumbani  ama  katika   mitandao  ya  kijamii.

Lakini  kuna  sababu  nyingine  ya hali  hiyo ya  kunyong’onyea: Baada  ya  miezi 12 ya  uhuru wa  kisiasa , Sudan  haijapiga  hatua  ambayo ilipigiwa  matumaini.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles