29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Stars yaenda Kenya na matumaini kibao

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ tayari kipo Kenya, kikisubiri kuumana na timu ya taifa ya nchi katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan), utakaofanyika kesho jijini Nairobi.

Kocha Msaidizi wa kikosi hicho, Juma Mgunda amesema wataingia uwanjani kuikabili Kenya na mfumo tofauti na ule walioutumia katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na matokeo kuwa suluhu.

Kikosi cha Stars, kiliondoka jijini Dar es Salaam jana, kikiwa na wachezaji 20 ambao walionekana kuwa na morali ya juu.

Akizungumza na MTANZANIA jana Mgunda alisema,  wanafahamu wapinzani wao watafunguka kwa sababu watakuwa wanahitaji ushindi, hivyo kwa upande wao watatumia mwanya huo kuwafunga.

Tunafahamu tutawakamata sehemu gani Kenya, sisi tutaingia uwanjani tukiwa na mfumo mpya wa kuwashambulia kwa kushtukiza.

Kwakua wao watafunguka sisi tutapata mwanya wa kuwafunga,” alisema.

Alisema hawana presha licha ya kuwa watakuwa ugenini, kwani wanaamini watapata matokeo na kuwapa furaha Watanzania.

Upande wake nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Kaseja, alisema hawafikirii matokeo ya  mchezo uliopita, badala yake wanaelekeza nguvu kuhakikisha wanashinda mchezo wa kesho.

“Hatuwezi kuangalia ya nyuma, kwa sasa tumejipanga kuwakabili wapinzani wetu Kenya, kama wao waliweza kupata suluhu kwetu na sisi tunaweza kupata ushindi kwao.

“Kocha ameangalia mapungufu na kuyarekebisha, pia ametuelekeza  cha kufanya ili  kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kusonga mbele,” alisema Kaseja na kuongeza.

“Tutapambana dakika tisini kuhakikisha Watanzania waliotupa dhamana ya kuwawakilisha wanapata furaha.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles